Search This Blog

Wednesday, March 7, 2012

EUROPEAN BIGGEST COMEBACKS: TIMU HIZI ZILIWEZA KUFANYA WALICHOSHINDWA KUFANYA ARSENAL JANA DHIDI YA AC MILAN.





DECEMBER 11 1985: REAL MADRID 4-0 BORUSSIA MONCHENGLADBACH (5-5 ON AGG., REAL MADRID WALISHINDA KWA MAGOLI YA UGENINI)


Real Madrid walikuwa wamefungwa 5-1 in Germany katika mechi ya kwanza, katika mechi ya raundi ya kwanza ya UEFA Cup , na mechi ya pili ingehitaji kitu cha kushangaza kuweza kubadilisha matokeo yende upande wa timu yenye mafanikio makubwa ziadi katika historia ya Eurpean Cup.
Kwa bahati nzuri kwa mashabiki wa Spain, hivyo ndivyo ilivyotokea, magoli manne kutoka kwa Jorge Valdano na Carlos Santillana mbele ya mashabiki 95,000 yalitosha kuivusha Madrid kuendelea mbele.
Santillana alifunga goli la mwisho katika dakika ya 88 na kusababisha uwanja kupasuka kwa shangwe za mashabiki kwa kuipeleka timu hiyo katika iliyofuata. Madrid walienda wakachukua ubingwa wa ligi hiyo kwa kuwafunga wajerumani FC Koln 5-1 katika fainali.


APRIL 27 2006: MIDDLESBROUGH 4-2 STEAUA BUCHAREST (MIDDLESBROUGH WAKASHINDA KWA 4-3)



Moja ya matukio ya kukumbukwa katika historia ya UEFA Cup katika miaka ya hivi karibuni ilikuwa kikosi cha Middlesbrough chini Steve McClaren ambao walienda mpka afainali kucheza dhidi ya Sevilla pamoja nakuwa nyuma kwa goli 3-0 katika mechi robo na nusu fainali.
Basel ndio walikuwa kwanza, wakipata uongozi wa 2-0 katika first leg in Switzerland. Kabla ya kupata goli jingine katika dakika ya 23 lilowaacha wageni hao wakiwa mbele kwa goli 3-0.
Lakini magoli mawili kutoka Mark Viduka na red card aliyopewa mchezaji wa Basel yalianza kurudisha matumaini. Jimmy Floyd Hasselbaink akafunga la 3 kabla ya Massimo Maccarone kuibuka shujaa na kupiga msumari wa mwisho katika dakika za nyongeza.
Boro fans waliwekwa tena katika wakati mgumu katika kipindi ambacho hakikuzidi mwezi mmoja baada ya kufungwa 1-0 mjni Bucharest na Steaua katika mechi ya kwanza ya nusu fainali.
Mechi ya pili ilianza kwa mshtuko kwa wenyeji waliojikuta wapo nyuma 3-0 on aggregate  katika kipindi cha dakika 25 za mchezo baada ya kutangulia kwa 2-0. Lakini waliibuka mashujaa tena kutoka wanaume wanaovaa jezi nyekundu, huku Maccarone akifunga goli la kwanza kabla ya mapumziko.
Viduka akafunga goli la pili kabla ya Chris Riggot kuitumia vyema krosi ya Stewart Downing na kufunga bao zikiwa zimebakiwa dakika 15 kabla ya kipenga cha mwisho.
Lakini alikuwa ni Maccarone tena aliyefunga goli la nne na kuufanya uwanja wa Riverside kulipuka kwa shngwe za hatari katika dakika za nyongeza za mchezo huo.
Kwenye fainali vijana hao waliangukia pua kwa kufungwa 4-0 na Sevilla, lakini hilo halikutosha kumnyima kazi Steve McClaren katika timu ya taifa ya England.

MARCH 18 2010: FULHAM 4-1 JUVENTUS (FULHAM WAKASHINDA KWA 5-4 ON AGGREGATE)



Comeback nyingine kwa timu ya Uingereza katika michuano ya ulaya, time hii walikuwa ni underdogs Fulham waliowaadabisha Juventus wakiwa Craven Cottage baada ya kufungwa 3-1 mjini Turin.
Kama ilivyokuwa kwa Middlesbrough dhidi ya Steaua Bucharest na Basel, wenyeji walianza kwa kufungwa goli la mapema na David Trezeguet.
Baada ya hapo watoto wa Mohamed Al Fayed walikuja juu huku Bobby Zamora na Zoltan Gera wakiongeza magoli kwa wenyeji huku Fabio Cannavaro akipewa kadi nyekundu kabla ya half time.
Penati iliyoleta utata katika kipindi cha pili ilifungwa na Gera na dakika 10 baadae Clint Dempsey alimaliza kazi kutupia msumari wa mwisho katika jeneza la bibi kizee cha Turin.

APRIL 6 2004: AS MONACO 3-1 REAL MADRID (5-5 ON AGG. MONACO WAKAPITA KWA MAGOLI MENGI YA UGENINI)



Huu ndio mchezo uliopelekea Monaco kufika nusu fainali ya Chamions league wakicheza na Chelsea (ambao waliwafunga na kwenda kucheza na Porto ya Jose Mourinho katika fainali na kufungwa.) lakini pia ndio mchezo uliosaidi a kuwafikisha katika hatua ya juu zaidi katika historia yao ya kushiriki UCL.
Wafaransa walikuwa nyuma kwa 4-2 on aggregate wakiwa wamefungwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu, na mambo yalitoka kuwa mabaya kuwa ovyo kabisa baada ya Raul kuwafungia Galacticos goli la kuongoza katika mchezo wa pili dakika ya 35.
Lakini shukrani kwa goli kutoka kwa nahodha wa Monaco Ludovic Giuly muda mchache kabla ya mapumziko , wenyeji wakarudisha matumaini katika kipindi cha pili.
Alikuwa mtoto wa wao wenyewe Madrid Fernando Morientes aliyepeleka kilio kwao, baada ya kufunga goli la pili kabla ya Giuly tena kufunga goli la 3 na kuwaondoa Madrid katika mashindano hayo.

APRIL 8 2004: DERPOTIVO LA CORUNA 4-0 AC MILAN (DEPRTIVO LA CORUNA WALISHINDA KWA AGGREGATE YA 5-4)



Wahispania walifungwa 4-1 katika mechi ya kwanza mjini Milan katika uwanja wa San Siro, lakini maajabu yalienda kutokea katika uwanja wa Riazor mpaka imeendlea kuwa ndoto itakayowasumbua Milan kwa muda mrefu.
Timu yao ikiongozwa na mshambuliaji Walter Pandiani akisaidiwa na Albert Luque ambao wote wawili walifunga magoli mawili kabla ya Juan Carlos Valeron kufunga kwa kichwa na kuwaweka Wahispania hao kuelekea kupita kwa magoli ya ugenini kabla ya mapumziko .
Lakini wenyeji walikuwa bado hawajamaliza, nahodha wa klabu hiyo Fran alipiga shuti kali ambalo lilmbabtitiza beki wa Milan na kumpita Dida kuingia katika wavu wa Milan, hivyo kumaanisha kwamba AC Milan walikuwa wametolewa katika michuano hiyo.






No comments:

Post a Comment