Search This Blog

Saturday, March 3, 2012

MIDO AWATOA YANGA CHAMPIONS LEAGUE



Goli la Mshambuliaji aliyewahi kutamba na vilabu mbalimbali Ulaya na kurejea nyumbani kwao Misri, Mido lilitosha kuwaondoa Yanga katika mashindano ya klabu bingwa Afrika.

Yanga wakimaliza mchezo wakiwa pungufu kufuatia kadi nyekundu ya Athuman Iddi Chuji katika dakika ya 55, walionyesha kiwango kizuri katika kipindi cha pili, huku safu ya ushambuliaji ikiwaangusha yanga jijini Cairo.

Zamalek wakiwa katika jiji lao la Cairo katika uwanja wa jeshi na wakicheza bila mashabiki walijipatia goli pekee la ushindi katika dakika ya 31 kupitia kwa mshambuliaji wake Mido.

Katika kipindi cha pili nusura Zamalek wapate goli la pili kufuatia penati waliyoipata katika dakika ya 74 na kukosa penati hiyo. Huku yanga wakipoteza nafasi katika dakika ya 46.

Kwa matokeo hayo Yanga wametolewa katika michuano ya klabu bingwa Afrika, huku Zamalek wakisonga katika raundi ya pili.

Kikosi cha yanga kilichoanza leo: Shaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Stephan Mwasika, Nadir Haroub, Athuman Iddi, Juma Seif, Omega Seme, Haruna Niyonzima, Jerry Tegete, Keneth Asamoah na Nurdin Bakari

1 comment:

  1. tutabadilisha makocha tutatafuta mchawi ni vipigo kwa kwenda mbele si yanga, si simba, si taifa stars wala timu yoyote itakayo fanikiwa hadi pale watanzania watakapo fanya maamuzi magumu ya kuitoa ccm madarakani ndipo watanzania tutakapo anza kutabasamu ktk soka vinginevyo kila mwaka tutakuwa tunawashutumu makocha, maandalizi mabovu, sasa tujiandae mwakani ooh taifa stars ivunjwe aaah wakowapi wale vijana wa kopa kokakola, kocha katusaliti kwanini hajampanga fulani na sababu chungu nzima mwisho wa siku tunaishia kipigo. Tutauzunguka sana mbuyu ccm ni sawa na hirizi mtu kajifunga kiunono halafu anaingia kanisani kumuomba mungu wapi na wapi. hapo maombezi hayapokelewi hata muumini angelia vipi. Wazambia wanafanikiwa kwa sababu wao wanafanya mabadiliko ya utawala na hilo husaidia kuondoa zana ya kulindana.

    ReplyDelete