Search This Blog

Friday, February 10, 2012

EXCLUSIVE: XHERDAN SHAQIRI AZITOSA UNITED NA LIVERPOOL AHAMIA BAYERN MUNICH


Shqiri anakumbukwa kwa alichowafanya Man United wakati wa mechi ya mwisho ya makundi ya UCL msimu huu.


Bayern Munich wamekamilisha usajili wa kiungo wa FC Basle Xherdan Shaqiri, ambaye alikuwa akiwindwa na Liverpool na Manchester United.

Kiungo huyo mwenye miaka 20 kutoka Uswiss alifaulu vipimo vya afya mjini Munich wiki hii.

The Bavarian wametangaza kwamba makubaliano rasmi yameshafikiwa na Basle na mchezaji mwenyewe, ambaye amesaini mkataba wa miaka 4, na atajiunga Bayern mwanzoni mwa msimu ujao.

“Tuna furaha sana kutangaza kwamba tumefanikiwa kumsaini Xherdan Shaqiri, moja ya wachezaji bora chipukizi barani ulaya.” Alisema mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Christian Nerlinger.

Kocha wa Bayern Jupp Heynckes anaagalia mbele kuja kufanya kazi na kinda hilo msimu ujao “Shaqiri atakiimarisha kikosi chetu msimu ujao kwa uwezo wake mkubwa alionao. Nimekuwa nikimtazama kwa muda mrefu sasa na nimekubali anaweza kuwa mchezaji muhimu katika timu yetu.”

Shaqiri atapambana na Bayern Munich wiki mbili zijazo akiwa na timu yake ya sasa FC Basle katika hatua ya 16 ya Champions league.
Ada ya uhamisho ya Shaqiri haijatajwa lakini inaaminika ipo karibu na euro million 10.

No comments:

Post a Comment