Search This Blog

Friday, February 10, 2012

ZAMALEK WAMEKATAA KUCHEZA MECHI MOJA YA YANGA.


Klabu ya Zamalek kupitia meneja msaidizi wa Klabu ya hiyo, Ismail Youssef amesema Zamalek imetupilia mbali maombi ya Yanga ya kutaka mechi kati yao ya Ligi ya Mabingwa kuchezwa moja.Yanga imekuwa ikihofia usalama wake kwenye mchezo wa marudiano uliopangwa kufanyika Cairo kutokana na tukio la vurugu za mashabiki nchini Misri zilizosababisha watu 74 kupoteza maisha jijini Port-Said.

“Yanga imeomba kucheza na sisi mchezo moja kwa sababu ya kuhofia usalama wao Cairo, lakini kanuni za CAF zinatutaka Zamalek kuthibitisha kwanza hilo,” alisema Youssef.

Alisema, "tumekataa pendekezo lao hilo na hatutakubali kunyimwa haki yetu ya kucheza nyumbani kama timu nyingine kwenye mashindano haya."CAF ndio watakaoamua kwamba mechi yetu ya nyumbani tutacheza hapa Cairo au uwanja mwingine kama wakiona hapa Cairo hapafai,"alisema Youssef.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Yanga,  Selestine Mwesigwa alisema yeye hana tatizo na mtazamo huo wa Zamalek kwa kuwa wao wanasubiri kauli ya CAF.

"Sisi tunasubiri kauli ya CAF, hatuwezi kuzungumza lolote kutokana na madai ya Zamalek," alisema Mwesigwa.

Tayari Shirikisho la Soka la Sudan limeonyesha nia ya kutaka kuwa mwenyeji wa mechi hiyo kwa kutuma maombi yao kwa CAF.Timu hizo zitakutana Februari 19 jijini Dar Es Salaam na zitarudiana wiki mbili baadaye huko Cairo. 

Wakati huohuo; Kocha wa Zamalek, Hassan Shehata amesisitiza kuwa ataendelea kubaki na timu hiyo na kukanusha madai kuwa alikuwa na mpango wa kwenda kujiunga na Ittihad Jeddah.

2 comments:

  1. Yanga waache uoga sasa kama walitaka mechi ichezwe moja haitachezewa hapa bongo sasa hawaoni kama na wao wataathirika?

    ReplyDelete