Search This Blog

Saturday, February 25, 2012

EXCLUSIVE: NAFASI YA NGASSA SEATTLE SOUNDERS YACHUKULIWA NA MKONGO - AAMBIWA AENDELEE KUSUBIRI.

Ngassa akiwa na kocha wa Seattle Sounders alipoenda kufanya majaribio nchini Marekani.


Hatma ya mchezaji wa kimataifa wa Tanzania na Azam FC Mrisho Ngassa kwenda kujiunga na timu ya Seattle Sounders imejulikana leo baada ya blog hii kuongea na Rahim Zamunda mmiliki wa African Lyon na mtu aliyehusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha Ngassa kwenda kufanya majaribio nchini Marekani mwaka Uliopita.


Imefahamika kwamba Ngassa ambaye ilisemekana amefanya vizuri katika majaribio yake nchini Marekani hivyo angejiunga na Seattle Sounders mwezi January mwaka huu, hatoweza tena kujiunga na timu hiyo baada ya nafasi yake kujazwa na mchezaji mwingine kutoka nchini Congo.

Rahim Zamunda akiwa na kiongozi wa Seattle Sounders alipompeleka Ngassa kwenda kufanya majaribio mwaka jana.



"Ni kweli Ngassa hakuweza kujiunga na Seattle Sounders kwa sasa baada ya nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine ambaye anacheza nafasi kama ya Ngassa uwanjani. Mcongo huyo nae alifanya majaribio na Seattle akafanya vizuri na kocha akapendekeza yeye ndio achukuliwe kwanza kabla ya Ngassa, ambaye ataendelea kuangaliwa kwa ukaribu na itakapotokea nafasi nyingine atachukuliwa kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Marekani. Hiyo ndio hali halisi ya mambo yalivyo katika sakata la Ngassa kwenda kucheza Seattle Sounders." - Alimaliza Zamunda.

No comments:

Post a Comment