Search This Blog

Saturday, February 25, 2012

HATIMAYE ARSHAVIN AONDOKA ARSENAL - ARUDI ZENIT KWA MKOPO


Andrey Arshavin hatimaye amekuwa chanzo cha habari nzuri kwa mashabiki wa Arsenal jana Ijumaa baada ya kuondoka Gunners kwa mkopo.

Mchezaji huyo aliye na rekodi ya kununuliwa kwa fedha nyingi kuliko wote katika historia ya klabu  amerudi katika klabu ya Zenit St Petersburg baada ya klabu hiy ya Russia kukubali kulipa ada ya mkopo ya  £1million na pia kulipa mishahara ya mshambuliaji huyo mpaka mwishoni mwa msimu.

Arshavin ambaye aliigharimu Arsenal £15million alipojiunga na klabu hiyo kutoka Zenit in 2009, alisema kupitia Twitter account : “Limeisha”

Baadae kupitia Sport-Express in Russia alisema: “Ijumaa ilikuwa siku ngumu sana, hakuna kilichokuwa kimeamuliwa mpaka dakika ya mwisho. Lakini naamini kutoka sasa kila kitu kitaenda vizuri. Nataka kucheza na nitafanya yote niyawezayo kuisadia Zenit kushinda taji la ligi.”

2 comments:

  1. A,aleykum kaka vp suala la Mohamed Bhinda ebu tusaidie ktk hili.

    ReplyDelete
  2. Du afadhali mshikaji ameenda mitaa ya kwao,ikibidi akapige misumari,by Yahya wa Dar.

    ReplyDelete