Search This Blog

Thursday, December 15, 2011

PAUL POGBA MBIONI KUONDOKA MANCHESTER UNITED


Kinda la klabu ya Manchester United Paul Pogba yupo tayari kuikacha ofa ya Sir Alex Ferguson na kufungua mazungumzo na Italian giants Inter Milan.

The French Teeneger, ambaye anatazamwa kama moja ya wachezaji wenye vipaji vikubwa walioandaliwa na Ferguson kwa ajili miaka ijayo, amekaribia kumaliza mkataba wake unaishia mwishoni mwa msimu, which means anaweza akakubaliana na klabu ya nje ya England mapema mwanzoni mwa mwaka ujao.

Washauri wa Pogba wamekuwa wakimtafutia soko kwa kila njia na Inter ndio wanaonekana kuongoza mbio za kutaka saini yake.

Fergie amekuwa akitumaini kwamba Pogba atakubali kuendelea kukaa OT, ambapo kwa sasa anaweza kutumika kama mbadala wa majeruhi Darren Fletcher na Anderson katika ngwe ya pili ya msimu.

However, camp ya Pogba na washauri wake, ambao pia wanamuwakilisha mchezaji wa Manchester City Mario Balotelli wanaonekana wakitaka mchezaji huyo aondoke Theatre of Dreams.

Ferguson anategemewa kumfungia kabisa vioo Pogba kama hatokubali kuwa commited na Man U, akimuacha nje ya kikosi kwa muda wote uliobakia wa mkataba wake.

United suspect Pogba tayari ameshafanya uamuzi wa mwisho kuondoka Old Trafford na tayari wanasemekana wameanza kumtafuta kuingo kinda mbadala wake ndani ya kikosi chao.

1 comment:

  1. shaffih kuna habari toka ndani ya united kua dogo huyu mkataba wake unaisha 2013 na huyu mwandishi kalipuka2 kama magazeti ya udaku coz everthing that happens within united is a big story whatever the rubish it is.Chela wa dom

    ReplyDelete