Search This Blog

Thursday, December 15, 2011

Tofauti ya tamaduni kati ya England na Italia Ndani ya uwanja

1) Italia, siku ya Jumapili watu huenda Kanisani, kisha wanakwenda katika mechi halafu wanakwenda nyumbani, wakati England watu wanaamka na kwenda baa halafu wanakwenda katika mechi kabla ya kurudi tena baa.

2) Italia mashabiki wanakula pasta na meatballs kisha wanashushia Wine nyekundu kabla ya kwenda uwanjani, wakati England, wanabugia Kababu na chips na kisha kujimwagia bia nyingi tumboni kabla hawajakwenda uwanjani.

3) Italia Polisi wanakuruhusu kulirushia basi la wachezaji machungwa, Uingereza utaishia Jela ukifanya hivyo…

4) Italia mashabiki wanajiheshimu wakienda ugenini, lakini wakiwa nyumbani wanakuwa wehu, wakati England mashabiki wanajiheshimu nyumbani wakienda ugenini wanageuka kuwa wehu wakubwa.

5) England, mashabiki wanakaa kwa amani katika viti vyao, wakati Italia viti vinatumika kama silaha.

6) England, maaskari waangalizi wa viwanja huwa wanatazama uwanjani, wakati Italia maaskari huwa wanatazama mechi inayoendelea.

7) England, kama unataka kununua kitu Fulani chakula inabidi unyanyuke na kwenda zako hoteli au baa iliyopo uwanjani. Italia unakaa hapo hapo ulipo huku ukimpigia kelele muuzaji ambaye anakuwa amesimama kando yako kwa mita 20 tu. Unawapa mashabiki wenzako noti yako mpaka inamfikia muuzaji. Hii ni kama uwanja wetu wa taifa vile…….

8) England, kama una nguvu, kasi na imara kuweza kucheza dakika 90 bila ya kusimama basi wewe unachukuliwa kama mchezaji mahiri hata kama una akili ndogo kama Punda. Italia, kama una akili na mbinu nzuri unachukuliwa wewe ni mchezaji mahiri hata kama una kasi ndogo kama Konokono.

9) England, kama SKY Sports wakisema Peter Crouch ni mchezaji bora duniani, nchi nzima inasikiliza na kuamini huku baadhi wakieneza maneno hayo, lakini kituo cha SKY Italia kikisema Simone Loria ni mlinzi bora duniani, nchi nzima inakata uhusiano wake na kituo hicho cha televisheni.

10) Italia, vitu kama kumvuta mchezaji mwenzako jezi, kujirusha, kumchezea mwenzako rafu mbaya, vinachukuliwa kama sehemu ya mchezo, wakati England vinachukuliwa kama ujeuri na mchezo usio wa Kiungwana

11) Italia, kulinda lango bado kunahitaji kucheza soka la akili, wakati England, kulinda lango ni kucheza vita na kwenda kinyume na utamu wa soka.

12) Italia, kama timu iko nyuma kwa mabao 3-0, wachezaji wote wanakata tamaa huku mashabiki wakiitukana timu nzima. Wengine wanakwenda kuvunja vioo vya mchezaji aliyecheza ovyo zaidi huku pia wakivamia mazoezi ya timu kesho asubuhi. England, timu hata kama imefungwa mabao 8-0, wachezaji wanaendelea kupigana uwanjani huku wakiufukuzia kila mpira. Mashabiki wataendelea kuwashangilia wachezaji wao bila ya kujali.

13) England, mwamuzi mbaya anahukumiwa kuwa amekosa ushindani, wakati Italia mwamuzi mbaya anaambiwa amechukua rushwa.

14) England mara baada ya mechi za mwisho zinapomalizika, asilimia 99 wanaonyesha ‘Highlights’ wakati asilimia 1 tu wanaonyesha uchambuzi. Italia wanatumia asilimia 1 kuonyesha highlights, na wanatumia asilimia 99 kufanya uchambuzi (slow-motion replays).

15) England, ni mara chache kumsikia Mwenyekiti wa Klabu akiongea kuhusu mpira. Wao wanajali biashara zao na kukaa mbali na vyombo vya habari. Italia, Marais wa klabu ni vichaa na kila siku wanatoa kauli za utata kwa vyombo vya habari. Mfano ni Rais wa klabu ya Palermo, Maurizio Zamparini ambaye haishiwi kauli za utata.

5 comments:

  1. Asilimia 75 zatamaduni za Italy, wabongo tunazo.

    ReplyDelete
  2. i like it,kweli kaka ww ni mgodi,itabidi utupe hii kwny sports extra leo na mbwiga mbwigane mkoma nyani mzee wa umateumate..,hahahaaa

    ReplyDelete