Search This Blog

Thursday, December 15, 2011

HIGUAIN AHITAJIKA CHELSEA KWA £30MILLION


Taarifa kutoka Daily mirror zinasema klabu ya Chelsea wanapanga kuzitumia pesa watakazopata katika mauzo ya wachezaji Nicolas Anelka na Fernando Torres kumnunua Muargentina Gonzalo Higuain kutoka Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa £30million.

Ingawa bado hawajaanza mazungumzo rasmi na Real Madrid , chanzo cha habari kutoka ndani ya The Blues kilisema kwamba wameshaonyesha nia ya kumuhitaji mshambuliaji huyo ili kuweza kukiongezea nguvu kikosi chao na kuweza kuhimili ushindani mkubwa uliopo msimu huu.

AVB, manager wa Chelsea anamuona Higuain kama suluhisho la tatizo la ushambuliaji linaloikumbuka timu hiyo kutokana na kiwango kibovu cha Torres, kuondoka kwa Anelka, akiwa na anabakiwa na Didier Drogba pekee ambaye nae katika siku za hivi karibuni ameonekana kuandamwa na majeruhi. Mshambuliaji mpya Romelu Lukaku bado anahitaji uzoefu ili kuweza kufanya vizuri katika mikikimikiki ya ligi kuu ya England.

Higuain inasemekana kutokuwa na furaha ndani kikosi cha Real Madrid kutokana na kuwa chaguo la pili la Mourinho nyuma ya in form Karim Benzema.

2 comments:

  1. KAKA HAPO NAZAZI SASA CHELSEA WATAKUA WAME PATA JEMBE ILA YASIJE KUA KAMA YA TORES MAANA KATIA AIBU YANI HATA YEYE ANAONA AIBU KUTOKA KWENYE KUFUKUZIA UFUNGAJI BORA MPAKA MKAA BENCHI BORA.NINOMA...JUMA YUNUS DSM

    ReplyDelete
  2. Kaka bado watakuwa hawajatibu coz con majembe nyuma yake Ndaki wa TEKU

    ReplyDelete