Search This Blog

Thursday, December 15, 2011

TOTTI: NAFIKIRIA KUONDOKA AS ROMA


Nahodha na kipenzi cha timu ya AS Roma Francesco Totti ame-react kwa hasira juu ya lawama anazozipata kutoka mashabiki wa timu yake hadi kufikia hatua ya kusema anafikiria kuihama klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa maisha yake yote.

The 35-year old forward amekuwa katika kiwango kibovu chini ya utawala wa kocha Luis Enrique msimu huu na mpaka sasa hajafunga goli hata moja, huku akikosa penati muhimu usiku wa Jumatatu katika droo ya 1-1 kati ya Roma na Juventus.

Roma walitumia pesa nyingi katika usajili kiangazi kilichopita, wakiwasajili wachezaji wenye makubwa wakiwemo washambuliaji wawili, Bojan Krkic na Pablo Osvaldo.

Akiongea na Sky Sport Italia kabla ya dinner ya klabu hiyo kuikaribisha krismasi Totti alisema: “Nimefikiria kuhusu kuondoka Roma, especially recently. Nimesikitika kwa kusikia taarifa ya zilitolewa na mashabiki wa Roma. Kama wana matatizo na mimi kuendelea kuwa hapa, nitaendelea kufikiria kuondoka.”

Totti alianza kuichezea Roma in March 1993, huku kocha wa zamani Vujadin Boskov akimchagua kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Brescia mechi ambayo Roma walishinda 2-0, kipindi hicho Totti alikuwa na miaka 16.

Mshambuliaji huyo kwa sasa anashikilia nafasi ya tano katika listi ya wafungaji bora wa muda wote wa ligi ya Serie A, akifunga magoli 207 katika mechi 481 mpaka sasa.

Roma wapo nafasi ya 10 in Serie A mpaka sasa na wanakabiliwa na mtihani mgumu kwenda kwa Napoli jumapili hii.

No comments:

Post a Comment