
2. WACHEZAJI WENGI WAMEJIJENGEA UMAARUFU KWA USTADI NA UFUNDI WA KUPIGA PENATI,KUNA KILA MTINDO WA KUPIGA PENATI AMBAO UMETUMIKA HADI KUFIKIA LEO LAKINI HAKUNA PENATI ITAKAYOFUNIKA ILE ILIYOPIGWA NA KIJANA AWANA THIAB WA UNITED ARAB EMIRATES.KIJANA HUYU ALIPIGA PENATI AMBAYO ILIMPA UMAARUFU ULIMWENGUNI KOTE AMBAKO PICHA ZAKE AKIPIGA PENATI ILE ZILIONEKANA . AWANA ALIPIGA PENATI KWA KUTUMIA KISIGINO HUKU AKIWA AMEMPA GOLIKIPA MGONGO. KWA BAHATI MBAYA REFARII HAKUONA KAMA AWANA AMEFANYA UUNGWANA , ALITAFSIRI KITENDO KILE KAMA UDHALILISHAJI WA MCHEZAJI NA MCHEZO WA SOKA KWA UJUMLA NA KWA HILO ALIMUONYESHA KADI NYEKUNDU .
KILICHOWASHANGAZA WENGI SIYO JINSI AWANA ALIVYOFUNGA BAO LILE BALI ILE HALI ALIYOKUWA NAYO BAADA YA KUFUNGA , HAKUONEKANA KUJAWA NA MSISIMKO KAMA INAVYOKUWA KWA WACHEZAJI WENGINE WANAPOFUNGA. KWA BAHATI MBAYA AWANA DIAB HAKUISHI MUDA MREFU KUSHUHUDIA JINSI UMAARUFU WAKE ULIVYOITEKA DUNIA KWANI ALIFARIKI DUNIA MIEZI MICHACHE BAADA YA TUKIO HILI KWA AJALI MBAYA YA GARI.
3. TUKIO LA TATU NI GOLI AMBALO JINSI LILIVYOFUNGWA HAKUNA ALIYESHUHUDIA AMBAYE ATAWEZA KUSAHAU KIRAHISI. BEKI WA TIMU YA FAGIANO OKAYAMA RYUJIRO UEDA ALIFUNGA BAO LA KICHWA KUTOKA NYUMA YA MSTARI WA KATIKATI YA UWANJA UMBALI WA KARIBU YADI 63 TOKA LILIPO GOLI . BAO HILI LILIINGIA KWENYE REKODI KAMA BAO LILILOFUNGWA TOKA MBALI ZAIDI KWA KUTUMIA KICHWA .
ENDELEA KUWA NASI MENGINE YATAFUATA MUDA SI MREFU!!!
No comments:
Post a Comment