Search This Blog

Thursday, November 17, 2011

BOBAN AITWA KWENYE KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS


28 WAITWA KILIMANJARO STARSK

ocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa ameteua wachezaji 28 kuunda kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji inatakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 25 mwaka huu. Wachezaji walioteuliwa ni Juma Kaseja (Simba), Deo Munishi (Mtibwa Sugar) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni Shomari Kapombe (Simba), Godfrey Taita (Yanga), Juma Jabu (Simba) na Paul Ngelema (Ruvu Shooting). Mabeki wa kati ni Juma Nyoso (Simba), Said Murad (Azam), Erasto Nyoni (Azam) na Salum Telela (Moro United). Viungo ni Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mwaipopo (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba), Haruna Moshi (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Rashid Yusuf (Coastal Union), Jimmy Shogi (JKT Ruvu Stars) na Mohamed Soud (Toto Africans). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Gaudence Mwaikimba (Moro United), John Bocco (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Daniel Reuben (Coastal Union) na Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada).

MAPATO STARS v CHAD

Pambano la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil- raundi ya mtoano kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Chad lililochezwa Novemba 15 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 78,389,000. Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,111. Viti vya kijani na bluu ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 2,000 ndivyo vilivyovutia mashabiki wengi ambapo walikuwa 23,748 ikiwa ni zaidi ya asilimia 80 ya mashabiki wote walinunua tiketi kwa ajili ya viti hivyo. VIP A ambapo ndipo kulikokuwa na kiingilio cha juu cha sh. 20,000, jumla ya mashabiki 187 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo. VIP B ambapo kiingilio kilikuwa sh. 10,000, mashabiki walionunua tiketi walikuwa 1,181. Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh. 5,000 kwa VIP C ambapo waliingia mashabiki 1,678 wakati mashabiki 2,319 walikata tiketi kwa viti vya rangi ya chungwa ambapo kiingilio kilikuwa sh. 3,000.

VIONGOZI WALIOCHAGULIWA KUONGOZA FAM

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM) ulifanyika Novemba 13 mwaka huu wilayani Rorya. Uchaguzi huo uliendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya FAM chini ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Viongozi waliochaguliwa kwa kuzingatia Katiba ya FAM na Kanuni za Uchagzui za wanachama wa TFF ni wafuatao; Fabian Samo amefanikiwa kutetea wadhifa wake wa Mwenyekiti huku Deogratius Rwechungura akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti. Wengine waliochaguliwa ni Mugisha Galibona (Katibu Mkuu), Samwel Silasi (Katibu Msaidizi), Evans Liganga (Mhazini), David Sungura (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), William Chibura (Mwakilishi wa Klabu) na Valerian Goroba (Mjumbe).

7 comments:

  1. soka la bongo bila kuwekeza kwa vijana hatutafika kokote, ni bora kutumuia mamilioni wanayopewa wachazaji wa taifa stars, kwenye timu ya vijana under 20, ila miaka michache ijayo tuwe na timu ya taifa yenye kueleweka kuliko ilivyo sasa, unakwenda kushabikia stars na presha juu,

    ReplyDelete
  2. all da best kili starz!!!

    ReplyDelete
  3. Jamani sioni umuhimu wa kuwaita wakina SAMATA na ULIMWENGU NA NIZAR,waacheni wacheze kwenye timu zao ili wajihakikishie namba,nyie tafuteni wachezaji wengine badala yao ili wawepo wazoee mazingira kuliko kung'áng'ania hao wanaotegemewa huko kwao. Mtasababisha wakose namba watakaporudi kwenye timu zao.Na pia viongozi wataona mnawa yeyusha kuwaitaita kila mara.
    Tafuteni vijana wengine ambao mnakuwa kama mmewekeza kwao.

    ReplyDelete
  4. Kwa nini mkwasa asiwaite angalau vijana hata saba kwenye kikosi chake kwaajili ya kuwapa uzoefu.hawa vijana watapata vp uzoefu pasipo unganishwa pamoja na hawa wakongwe.jamani kweli tutapata mafanikio namna hii.Soka letu litazidi kurudi nyuma badala ya kwenda mbele.hakukuwa na haja ya kuwaita wakina Nizar.

    ReplyDelete
  5. Ni nafasi adimu kwa Mkwassa kuonyesha kuwa makocha wazawa wakiwezeshwa wataweza.

    ReplyDelete
  6. Mwenye jukumu la kuwekeza kwa vijana ni Poulsen na siyo tim hii ya kina Mkwasa coz wao cyo Makocha wa kudum wa hii tim hivyo ni vyema kuchukua wazoefu wakafanya kazi coz muda wenyewe mfupi ila kwa tim ya Taifa nakubaliana na point ya kuwekeza kwenye vijana...

    ReplyDelete
  7. Nizar khalfan atakuwepo kwenye chalenji? kwani si zani kama inatambuliwa katika kalenda ya FIFA sasa tusiite m2 tu kwa umaarufu wa jina wakati wako wengi wa kucheza nafasi yake au kumtaja halafu akakosa ruhusa ya Club kwa kua haiko kwenye Ratiba ya FIFA

    ReplyDelete