Search This Blog

Thursday, November 17, 2011

SUAREZ ASHTAKIWA NA FA KWA KUTOA MANENO YA KIBAGUZI DHIDI YA EVRA


Mshambuliaji wa ki-uruguay Luis Suarez anayeichezea klabu ya Liverpool ameshtakiwa na FA kwa tuhuma za kumtolea maneno ya kibaguzi Patrice Evra.

Mshambuliaji alishutumiwa na mlinzi wa Manchester United mara tu baada ya mchezo dhidi ya timu zao ulioisha kwa matokeo ya sare ya 1-1 mwezi uliopita.

Akiongea baada ya mchezo , Evra aliiambia kituo cha matangazo cha kifaransa: “Kuna camera. Unaweza kuona Suarez akiniambia neno la kibaguzi zaidi ya mara 10.”

Lakini Suarez alipinga madai hayo ya Evra, akisema: “Nimekasirishwa sana na shutuma hizi za ubaguzi wa rangi. Ninachoweza kusema kwamba siku zote nimekuwa nikiheshimu kila mtu. Wote tupo sawa. Naenda uwanjani kucheza mchezo ninaofurahia na sio kuleta mitafaruku.”

Hata baada ya kujitetea chama cha soka cha FA kimeona kuna kesi ya kujibu kwa Suarez, ikiwa ni muda mchache tangu Raisi ya FIFA Sepp Blatter kukaririwa akisema hakuna ubaguzi wa rangi ndani ya dimba la soka.

No comments:

Post a Comment