Search This Blog

Thursday, November 17, 2011

Binafsi sina lengo la kuwa mwanasiasa- Aboutraika..


Number 10-Unaelezeaje historia yako kifamilia na ulianzaje soka lako?

Aboutraika-Kiukweli mimi nimetokea kwenye familia masikini , kama ilivyo kwa familia nyingi Misri, nilipata tabu sana utotoni , niliwahi kufanya kazi kwenye kiwanda cha matofali nikiwa na umri wa miaka 12 ili kuisadia familia yangu katika kulipa ada ya shule na pia nilianza kujitegemea nikiwa na umri mdogo sana .Wazazi wangu walifanya juhudi kubwa sana kunikuza na kunilea na tabu tulizopata utotoni zimenisaidia san kufika hapa nilipo leo.Nilianza kucheza soka mitaani na vijana wenzangu nikiwa mdogo hadi hapo jirani yetu mmoja aliponiona na kunipeleka timu inayoitwa Tersana huko Misri kwa ajili ya majaribio , nilicheza huko kwa miaka 12 hadi hapo nilisajili El Ahly ambao nimekuwa nao kwa miaka nane sasa.

Number 10-Siku zote umekuwa ukifunga mabao muhimu kwenye nyakati muhimu za mechi,unawezaje kufanya hivyo?

Aboutraika
-Ni zawadi toka kwa Mungu kusaema kweli, kwa yote ninayofanya siwezi kuamua kufunga bao la ushindi au la kusawazisha au kufunga kwenye dakika za majeruhi , ni zawadi toka kwa Mungu na natumaini zawadi hii ntaendelea kuwa nayo.

Number 10-Ulicheza dhidi ya Brazil na Italia mwaka 2009.Ulijisikiaje kucheza kwenye kiwango cha juu kama hivyo?
Aboutraika
-Ilikuwa kitu kizuri sana kwangu.Kiwango ambacho unajihisi upo ukiwa unacheza kwenye michuano kama ile ni kikubwa sana na unaona mwenyewe unapokuwa uwanjani, ni kiwango cha juu sana ambacho kilitupa nafasi ya kuonekana dunia nzima kama timu na kama nchi, nadhani Misri ina vipaji vya kutosha kupambana na timu kama Brazil na Italia .

Number 10-Ulikuwa unawaza nini ulipokuwa unacheza mechi hizi?

Aboutraika-Tulifikiri kuwa hatuna chochote cha kupoteza kama timu,sio kama tunacheza mechi hizi kila siku hivyo nafasi zote chache tunazopatra tunazitendea haki kadri tuwezavyo, ilikuwa nafasi ya kuonyesha uwezo wetu, hakuna aliyetaraji kutuona tukiwa washindi ila tulitumai kuonyesha dunia nzima sisi ni kina nani na soka letu lilipo.

Number 10-Misri haijacheza kombe la dunia tangu mwaka 1990, unaweza kutueleza kwanini?

Aboutraika-Wapinzani wetu wanasema kuwa tunacheza soka zuri na bora kuliko timu nyingi Afrika , lakini huwa tunafanya hivyo pale tunapokuwa pamoja kwa muda mrefu kitu ambacho ni cha kweli, kwa mfano kwenye kombe la mataifa ya Afrika ambako tunakaa pamoja kwa muda mwingi lakini huwa tunakaa kambini kwa siku tatu tu kabla ya mechi za kufuzu kombe la dunia na umeona tofauti ilipo kwenye mataifa ya afrika tumefanyaje na kwenye kombe la dunia tumefanyaje.

Number 10-Umewahi kupoteza matumaini juu ya kucheza kombe la dunia katika maisha yako?


Aboutraika-Inakuwa vigumu sana kwangu kushiriki kombe la dunia , kwanza kwa sababu ya umri wangu, lakini nadhani kwa kila mafanikio yanapokosekana uzoefu unaongezeka , inabidi tujikakamue na na kupigana huku tukiwa na matumaini kuwa siku yetu itakuja na sisi tutacheza .

Number 10-Bado una mawazo kuwa mchezo wa soka unaunganisha watu?

Aboutraika-Hakika , mchezo wa soka unaunganisha watu na unasaidia kwenye vita dhidi ya umasikini. Mbali na kucheza soka na kufunga magoli mchezo huu unajenga maadili ya watu , sisi tunawapelekea watu ujumbe na misingi ya kimaisha kwa watu , huu ni mchezo ambao unapeleka ujumbe wa masuala ya biashara na hata siasa ni mchezo ambao unavuka zaidi ya uwanja.

Number 10-Imani yako ina umuhimu gani kwako?

Aboutraika-Mimi ni muislamu na ninaona sifa kuwa muislamu .Unapata nguvu za mwili kutokana na kufanya mazoezi lakini nguvu ya kiimani inatoka kwa Mungu, Mungu anakupa nguvu ya maisha,uhusiano wako na Mungu ndio unaokupa maisha na ndio kitu cha muhimu kuliko kila kitu katika maisha, ni mahesabu rahisi sana Mungu alituumba na roho na mwili lakini roho haiwezi kuwa na nguvu bila ya kupewa nguvu hiyo na Mungu, nadhani Mungu anapaswa kutafutwa na kila mtu ulimwenguni.

Number 10-Kuna picha inakuonyesha wewe ukipiga magoti kuswali kwenye mahali Fulani pale Tahrir siku ambayo Hosni Mubarak aliachia ngazi, kuna kitu chochote hapa?

Aboutraika-Hakuna chochote pale ambacho kina maana kubwa , nilikuzwa kwa kuelekezwa kuwa kuna mabaya na mema,nimepewa zawadi na Mungu na siku zote naunga mkono kilicho sahihi.Unaweza kuwa kwenye baya au kwenye jema au unaweza kuwa katikati ya mambo yote yanayotokea au unaweza kuunga mkono yanayotokea . Baada ya hotuba ya mwisho ya Mubarak, siku moja kabla ya kuachia ngazi,nilihisi kuwa kuna hisia kubwa za hasira na kukata tama miongoni mwa watu wote hasa wale waliokuwepo pale Tahrir Square,nilikuwa na lengo la kuwanyanyua watu wangu na kuwapa moyo kuwa kuna mema yanakuja.

Number 10-Unadhani ungeweza kujiunga na na waandamanaji wakati vugu vugu lilipoanza ?

Aboutraika-Nadhani ningejiunga na waandamanaji mwanzoni kama ningepata nafasi ya kufanya hivyo , niliwahi kufikiri kujiunga na waandamanaji mwanzoni na siku zote nilipowaza nilipata wazo ambalo lilinipa sababu ya kungoja .

Number 10-Uliwahi kuwaza kuwa ungeunga mkono mapinduzi halafu inatokea yakafeli ungejiweka kwenye wakati mgumu katika maisha yako ya soka?

Aboutraika-Hapana , sijawahi kufikiria hivyo hata siku moja . Ninaaamini kuwa maishani kuna wakati unapaswa kuwa na msimamo na unachotaka na hupaswi kufanya mahesabu kwenye msimamo huo na hupaswi kuwaza matokeo mabaya akilini mwako , kaka unaamini kuwa unachounga mkono ni sahjihi basi kifanye pasipo woga.
Number 10-Ulijisikiaje kuona Mubaraka akiachia ngazi mwisho wa siku ?

Aboutraika-Kama mtu yoyote wa Misri nilipata tabu kutokana na rushwa ambayo imepoteza maisha ya watu wengi na rasilimali pia, nilipoteza haki zangu kwa kiasi kikubwa kutokana na rushwa.

Number 10-Je una malengo ya kujiunga na siasa?

Aboutraika-Hapana mimi ni mtu wa vyama vyote , naamini mtu yoyte anaweza kuitumikia nchi yake na mtu yoyote mwenye malengo mazuri na nchi yangu nitamuunga mkono ila binafsi sina lengo la kuwa mwanasiasa.

No comments:

Post a Comment