Search This Blog

Thursday, November 17, 2011

NAMIBIA YAINGIA MICHUANO YA CHALENJI



Release No. 116

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Novemba 16, 2011

Namibia itashiriki michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza Novemba 25 mwaka huu ikiwa timu mwalikwa baada ya Eritrea kujitoa. Hivyo Namibia inaingia moja kwa moja katika kundi A ambalo lina mabingwa watetezi Tanzania Bara, Rwanda na Djibouti. Pia ratiba ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia ya Tusker imetangazwa rasmi leo (Novemba 16 mwaka huu) ambapo mechi zote zitachezwa Dar es Salaam baada ya Mkoa wa Mwanza kushindwa kutimiza masharti iliyopewa ili nayo iwe kituo cha michuano hiyo. Mechi mbili zitachezwa kwa siku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam isipokuwa Novemba 26 mwaka huu ambapo kutafanyika uzinduzi rasmi saa 10 jioni kwa mechi kati ya Tanzania Bara na Rwanda. Novemba 25 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Burundi na Somalia (saa 8 mchana) na Uganda na Zanzibar itakayoanza saa 10 jioni. (Ratiba yote ya mashindano imeambatanishwa)


MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI


Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro), Charles Boniface Mkwasa kesho (Novemba 17 mwaka huu) saa 6 mchana atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika ofisi za TFF ambapo pamoja na mambo mengine atatangaza kikosi kitakachotetea Kombe la Chalenji.


Boniface Wambura Mgoyo

Ofisa HabariShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment