Search This Blog

Friday, October 28, 2011

WAMBURA: NAENDA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YANGU


Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara(FAM) kabla ya kuenguliwa katika kinyang'anyiro hicho, Michael Wambura amesema amemwandikia barua Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Alfred Tibaigana ili kumweleza kile alichodai kutopokelewa kwa rufaa yake aliyowasilisha kwenye ofisi za shirikisho hilo.

Wambura anaishutumu TFF kukataa rufaa yake kwao juzi akipinga kuondolewa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa FAM na kamati ya uchaguzi ya TFF iliyokutana jijini Dar es Salam wiki iliyopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Wambura alisema kuwa amefikia uamuzi wa kumuandikia barua Tibaigana kujua kama kamati yake ina uwezo wa kusikiliza rufaa yake au haina kabla ya kuamua kuchukua hatua nyingine anazofikiri zinamfaa.

Alisema kuwa,hilo limekuja baada ya jana TFF kwa mara nyingine kukataa kupokea kiasi cha Sh 300,000 kama ada ya rufani.Wambura alisema kuwa endapo Tibaigana atamjibu kwamba hana uwezo wa kusikiliza sakata lake, anatarajia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa lengo la kupata haki yake.

"Jana nimepeleka tena Sh,300,000 kama ada ya rufani pia wamekataa, baada ya hapo niliamua ni kwenda kutumia kwa njia ya benki na kisha nikawapelekea risiti ambayo pia wamekataa na nimeamua kuwatumia kwa Fax.

"Sasa hivi nimemwandikia barua Tibaigana kumweleza kuhusu kilichotokea ni matumaini yangu atanijibu haraka na kama ataniambia hata uwezo wa kusikiliza rufaa yangu Jumatatu nitakwenda kutafuta haki mahakamani," alisema Wambura.

Kamati ya uchaguzi ya TFF ilimwondoa Wambura kwa madai ya kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA)inayozuia masuala ya soka kupeleka mahakamani ikidai aliwahi kwenda mahakani kuishtaki Simba.

2 comments:

  1. Hivi wambura mbona king'ang'anizi sana. Hivi kuna nini huko TFF kunakomyima usingizi. Huyu jamaaa nimeanza kumuogopa. Halafu mambo ya mahakamani sio kabisa. Hivi kwa mfano wambura umekuwa mwenyekiti wa TFF, wadau tutajifunza nini kwako ikiwa nyuma ulikuwa mtu wa kwenda mahakamani ili hali unajua ni kinyume na taratibu za FIFA. Hatutaki kurudi enzi za kina ndolanga. Kama unataka kuisafisha TFF, nafikiri kuingia huwezi, but tumia vyombo vya habari funguka , anika uozo wao halafu wapiga kura watatoa hukumu.

    ReplyDelete
  2. Kwa nini wanamzuia jamaa ,kwa nini wasimwache agombee wapiga kura ndio wamkatae.TFF ya sasa ya kina Ndolanga ziko sawa sawa

    ReplyDelete