Search This Blog

Friday, October 28, 2011

TIMBE ASHIKILIWA HOTELINI, ADAIWA FEDHA ZA MALAZI.


Kocha aliyefungashiwa virago na klabu ya Yanga, Mganda Sam Timbe, amejikuta katika hali ngumu baada ya kung’ang’aniwa na uongozi wa hoteli aliyokuwa akiishi jijini Dar es Salaam kutokana na deni linalozidi Sh. milioni 19.5.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa hoteli ya Markham iliyopo Mikocheni zinaeleza kuwa Timbe ameshikiliwa ili kuishinikiza Yanga iliyompangia hotelini kulipa deni hilo linalotokana na malazi ya dola za Marekani 75 kwa siku (Sh. 128,576) pamoja na huduma nyingine ambazo zimelimbikizwa na Yanga tangu katikati ya Juni.

Meneja wa hoteli hiyo aliiambia blog hii jana kuwa uongozi wa Yanga ulimlipia Timbe kwa mwezi mmoja tu na tangu hapo hawajalipa tena na kuacha deni hilo liongezeke kila uchao.

"Tunajua si Timbe ambaye anatakiwa kutulipa fedha hizi, lakini tumeamua kushikilia hati yake ya kusafiria na tutaendelea kumdhibiti ili Yanga ambao ndio waliompangia watulipe fedha zetu," alisema meneja huyo.

Uongozi wa Yanga ulikiri jana kuwa ni kweli unadaiwa na hoteli waliyompangia Timbe na kudai kuwa wapo katika mchakato wa kuwalipa fedha hizo.

"Sisi (Yanga) tumefanya biashara na makampuni mbalimbali na hakuna iliyowahi kukimbilia kwenye vyombo vya habari kama hawa wenzetu. Tunawasiliana nao kila wakati na kuwaahidi kuwalipa fedha hizo, lakini tunawashangaa kwa hatua yao hii… ni kweli wanatudai na tupo kwenye mchakato wa kuwalipa," Afisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu.



No comments:

Post a Comment