Search This Blog

Friday, October 7, 2011

KASEBA AMTAKA TENA CHEKA


Wiki moja baada ya kushinda pambano lake dhidi ya Maneno Osward bondia Japhet Kaseba amesema kwa sasa yupo tayari kurudiana na Francis Cheka muda wowote.

Kaseba ameliambia gazeti hili kuwa kipindi alipopigana na Cheka na akapigwa kwa KnockOut alikuwa hana uzoefu, lakini sasa amejipanga na ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

Alisema alikuwa akicheza ngumi, kisha akahamia katika Kickboxing, alipoamua kurudi katika ngumi ndipo muda mfupi akapangwa kucheza na Cheka hivyo hakuweza kumhimili.

Alisema kwa sasa amejiimarisha zaidi na yupo tayari kupigana na bondia yeyote yule.

Alisema ushindi alioupata mwishoni mwa wiki, alipocheza na Maneno Oswald ni ushahidi tosha kuwa anaweza kupambana na hivyo atamkabili Cheka bila matatizo.

“Mimi kwa sasa ninahitaji kukutana na yeyote yule na nina uhakika kuwa nitashinda kwa KO ni suala la kutafuta promota tu,” alisema Kaseba.

Cheka mwenye maskani yake mkoani Morogoro amekuwa tishio katika mchezo wa ngumi na kuibuka na ushindi katika kila pambano analocheza.

No comments:

Post a Comment