Search This Blog

Friday, October 7, 2011

TAIFA STARS YAONDOKA, KADO ATEMWA


Siku chache baada ya kocha wake Sam Timbe kusema anacheza chini, golikipa Shaaban Kado na ameachwa katika katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 21 waliokuwemo katika msafara wa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ kwenda Morocco kwa mchezo wa mwisho kuwania kufuzu fainali za Afrika.

Kado ambaye aliitwa na kocha Jan Poulsen katika kikosi cha mwanzo na kusababisha malalamiko kutoka kwa wadau wa soka kwa madai hakuwa kwenye kiwango kizuri kama ilivyo kwa Mwadini Ally wa Azam, ameshindwa kupita katika chujio la wachezaji 21 waliotakiwa kwenda Morroco.

Nae ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kuwa Taifa Stars ilitarajiwa kuondoka jana jioni kwa ndege ya Qatar Airways kwenda Morocco kwa ajili ya mechi dhidi ya wenyeji ambayo itachezwa Jumapili wiki hii.

Alisema msafara wa Stars unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Wallace Karia na una wachezaji 20, benchi la ufundi lina watu sita chini ya Kocha Mkuu Jan Poulsen.

“Naibu Mkuu wa Msafara ni Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Alhaj Haji Ameir.

“Wachezaji ni Juma Kaseja, Shabani Dihile, Erasto Nyoni, Idrisa Rajab, Aggrey Morris, Juma Nyoso, Nadir Haroub, Henry Joseph, Nurdin Bakari, Shabani Nditi, Jabir Aziz, Mrisho Ngasa, Ramadhan Chombo, Abdi Kassim, Mbwana Samata, Dan Mrwanda, Mohamed Rajab, John Bocco, Hussein Javu na Nassoro Cholo.

“Mbali ya Poulsen, wengine kwenye Benchi la Ufundi ni Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Juma Mwankemwa (Daktari wa Timu), Alfred Chimela
(Meneja Vifaa) na Leopold Mukebezi (Meneja wa Timu).

Kwa mujibu wa Wambura, Stars itarejea Oktoba 11 mwaka huu saa mbili asubuhi.

No comments:

Post a Comment