Search This Blog

Friday, October 21, 2011

DANNY MRWANDA: T.F.F IACHE UBABAISHAJI


Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya Tanzania-Taifa Stars, na klabu ya DT Long An, Vietnam, Danny Mrwanda, amelitaka Shirikisho la soka Nchini (TFF) kuwa makini linapofanya mawasiliano ya kuwaita wachezaji wanaocheza soka nje kuja kujiunga na Stars.

Lakini kauli yake ilipingwa na TFF kupitia msemaji wake, Boniface Wambura alipokuwa akiongeaa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Mrwanda alishutumiwa na TFF kwa kitendo cha kuchelewa kuripoti kambi ya Stars ilipokuwa ikijiandaa kucheza na Morocco mechi ya mwisho kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.

Akiongea juzi, Mrwanda alisema wakati TFF ikituma taarifa kwenye klabu yake kumtaka kuja nchini, yeye wakati huo tayari alikuwa nchini kwa shughuli zake binafsi.

"Nilipewa taarifa na uongozi wa klabu (DT Long An, Vietnam) nikiwa nchini kwamba natakiwa nijiunge na wenzangu kwenye timu ya Taifa," alisema Mrwanda.

Mrwanda anasema alishangazwa na TFF kutompa taarifa za kuitwa kwake Stars, kwani mbali na kutoa taarifa kwa mwajiri wake pia, TFF ilikuwa na kujumu la kumfahamisha na yeye.

Mrwanda alisema kinachotakiwa kufanywa na TFF ni kuhakikisha mchezaji anapata taarifa mara tu wanapowasiliana mwajiri wake, na si tu kusubiri klabu ndio impe taarifa.

Aidha Mrwanda aliilalamikia TFF kwa kushindwa kumsaidia kupata visa kama ambavyo aliahidiwa na Mkurugenzi wa mashindano ambaye hakumtaja jina.

"Tangu turudi toka Morocco sijaondoka kwa vile visa yangu imeisha. Waliahidi wangenisaidi lakini mpaka sasa kimya," alisema Mrwanda.Kwa upande wake, Wake Wambura alisema walipeleka taarifa mapema kwenye klabu yake wakiwa na imani kwamba, pia taarifa hizo zitamfikia Mrwanda.

"Taarifa zilikwenda, na kweli huenda hakuwepo Vietnam wakati huo, lakini uongozi wa klabu yake haukutupa taarifa," alisema Wambura.

Akiongea kuhusu suala la visa, Wambura alisema suala hilo si jukumu lao kama TFF.
"Hatuhusiki kwenye hilo, ni jukumu la mchezaji mwenyewe kutafuta visa, labda kama anataka kusaidiwa nyaraka na si vinginevyo."
<!--[if !supportLineBreakNewLine]-->
<!--[endif]-->


No comments:

Post a Comment