Search This Blog

Friday, October 21, 2011

BASENA: T.F.F BADILISHENI MFUMO WA RATIBA YA LIGI -INACHOSHA


Kocha wa wekundu wa msimbazi Simba, Mganda Moses Basena amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), kuangalia upya upangaji wa ratiba za mechi za Ligi Kuu kwa madai kuwa inawachosha na kuwaumiza wachezaji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Basena alisema, TFF inapaswa kupanga ratiba itakayotoa nafasi kwa timu kucheza mechi moja kisha ikapata muda wa kupumzika kabla ya kucheza mechi nyingine.

Alisema kama hilo litazingatiwa, kutasaidia timu kuepuka tatizo la majeruhi mfululizo kama ambavyo imetokea kwenye kikosi chake siku za karibuni.

"Sioni sababu ya kucheza mechi mfululizo tena za ligi tu, mimi nafikiri shirikisho linapaswa kuliangalia hili kwa umakini vinginevyo tutakuwa tunawaumiza wachezaji kila kukicha.

"Ebu angalia, mfano tumecheza mechi ngumu leo, na baada ya siku tatu tunacheza mechi nyingine. Hii ni sahihi kweli," alihoji Basena.

Basena kocha msaidizi wa zamani timu ya taifa Uganda, The Cranes, alisema ni makosa kulinganisha mazingira ya ligi ya Tanzania na zile za Ulaya.

"Ligi za Ulaya ni za kulipwa, pia klabu zinashiriki mashindano tofauti na si ligi pekee.

"Mazingira yao ni tofauti na sisi, hivyo ni makosa kulinganisha ligi za kule na huku,"alisema Basena.

Akizungumzia suala hilo, Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema: "Hilo ni suala la kiufundi zaidi na wahusika ni Idara ya Ufundi ambao wana mamlaka ya kupanga ratiba."

Mkurugenzi wa ufundi wa T.F.F Sunday Kayuni was nowhere to be found kuelezea kuhusu shutuma za Basena.

No comments:

Post a Comment