Search This Blog

Tuesday, August 30, 2011

UHAMISHO WA MKOPO WA LUKAKU KWENDA STOKE CITY WASHINDIKANA

Stoke City wamekataliwa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji mpya wa Chelsea Romelu Lukaku.

Straika huyu wa kibelgiji ambaye amejiunga na The Blues kwa ada ya uhamisho ya £20m kutoka Anderlecht mapema mwezi huu lakini ana mpambano mkali wa kugombea namba kwenye kikosi cha kwanza Stamford Bridge.

Boss Andre Villas Boas alikuwa tayari kumpeleka kinda huyo Britannia Stadium kwa miezi 6 ili aweze kumrudisha mshambuliaji katika mzunguko wa pili wa msimu, lakini sheria za premier league zinasema mchezaji aliyenunuliwa na timu moja haruhusiwi kuuzwa kwa mkopo kwenda klabu nyingine katika wakati mmoja wa usajili (transfer window).


Huku Didier Drogba akitegemewa kuondoka mwezi January kwa ajili ya African Cup of Nations, Lukaku ndio anatajwa kuchukua nafasi yake na ndio maana AVB alikuwa tayari kumtoa kwa mkopo wa miezi 6 tu.

No comments:

Post a Comment