Search This Blog

Wednesday, August 31, 2011

COUNTDOWN YA KUFUNGWA KWA DIRISHA LA USAJILI NANI ANAENDA WAPI FUATILIA


ELIA AJIUNGA JUVENTUS

Mkataba wa miaka 4 kwa winga wa kiholanzi, na kibibi kizee cha Turin watawalipa Hamburg €9m kama ada ya uhamisho uliotangazwa rasmi leo.

Juventus wameendelea kukimairisha kikosi chao chini Antonio Conte baada ya kufanikiwa kumsajili Eljero Elia kutoka Hamburg kwa gharama €9m ambayo inaweza kuifikia €10m.

Elia, 24, ameshawasili Turin tangu jana jioni na leo atafanyiwa vipimo kabla ya kurejea kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uholanzi.


PAVLYUCHENKO AOMBA KUONDOKA SPURS

Yakiwa yamebaki masaa mahache kabla ya dirisha usajili kufungwa Roman Pavlyuchenko amewashangaza Tottenham baada ya kuondoka klabuni hapo.

Mrussia huyo ambaye alikuwa anategemewa kusaini mkataba mpya msimu, lakini sasa ameamua kubadili mawazo baada ya kusajiliwa kwa Emmanuel Adebayor White Hart Lane.

“Wakala wangu yupo London, amekutana na mwenyekiti Daniel Levy kujaribu kutafuta namna ya kuondoka, lakini mpaka sasa bado hakuna makubaliano.Tulitoa wazo la kuniruhusu kuondoka kwa mkopo kwa miezi 6 lakini Levy amekataa.

“Nafahamu Sunderland wamekuwa wakinihitaji, nasubiri kuona itakuwaje.Nchini England maajabu yanatokeaga kwenye siku ya mwisho ya usajili hivyo kuna tumaini japo sio kubwa.” Roman Pavlyuchenko.



REDKNAPP: MODRIC ANABAKI, NAMTAKA CAHIL AND PARKER

Asubuhi ya mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa saa 6 usiku leo, Harry Redknapp amesisitiza kwamba Luka Modric anabaki White Hart Lane.

Chelsea ambayo bado walibaki japo namatumaini kidogo ya kiungo huyo wa Croatia, lakini Redknapp leo asubuhi amemwaga sumu kabisa katika dili hilo: “Nina uhakika asilimia million Modric atabaki.” Aliiambia Sky Sports News.

Pia taarifa kutoka upande wa Tottenham zinasema kuwa timu hiyo imeweka mezani ofa ambayo inajumuisha pesa pamoja na kuwatoa wachezaji David Bentley na Sebastian Bassong kwa Bolton ili kuweza kumsainisha Gary Cahil mwenye thamani ya £17m.





Ingawa zimeendelea kutoka kauli za kukatisha tamaa ya usajili wa Wesley Sneijder kutoka kwa pande zote za Inter Milan na Man United, lakini sasa tukiwa na tumebakiwa na masaa machache kufikia kufungwa kwa dirisha la usajili barani ulaya, gazeti la Daily Star la nchini Uingereza linaripoti kuwa kiungo huyo wa kiholanzi anaweza kuwa mchezaji wa United muda wowote kabla ya saa sita kesho.

Taarifa zinasema mazungumzo kati ya timu ya wawalikishi wa Sneijder na United wamefanya mazungumzo na kuafikiana mshahara wa £190,000 kwa wiki ili mchezaji huyo atue @ Old Trafford.

Pia Daily Star imethibitisha kuwa Inter Milan wamewaambia United wapo tayari kushusha ada ya uhamisho kwa ajili ya Sneijder baada ya kufanikiwa kumsaini Diego Forlan huku wakiwa katika hatua za mwisho za kumsaini kiungo wa kiargentina kutoka Lazio Mauro Zarate.

Jana Kocha msaidizi wa United alikiri kuwepo kwa uwezekano wa Sneijder kutua Theatre of Dreams, alisema: “Penye nia siku zote kuna njia.Kama klabu tunamhitaji na mchezaji pia anataka kuja, hivyo lolote linawezekana.Mchezaji mwenye kariba ya Sneijder atatufaa vizuri sana.”



CHELSEA WATUMA OFA YA £30M KWA RIBERY

Chelsea wametuma ofa ya £30m kwa ajili wa star wa kifaransa anayeichezea Bayern Munich Frank Ribery.

The Blues boss Andre Villas-Boas ameamua kumgeukia Ribery katika kumsaka kwake world class playmaker baada ya kushindwa kumsaini Luka Modric kutoka Spurs, lakini Bayern Munich wameshaweka wazi hawatoijadili ofa isiyozidi £36m.Chelsea wapo tayari kumpa mkataba wenye thamni ya £10m kwa mwaka Ribery.

Sasa AVB lazima aamue ama kukubali kulipa pesa waitakayo Bayern auamkose mchezaji huyo.

Ribery ambaye alisajiliwa na Bayern akitokea Mersaille kwa ada ya £22m mwaka 2007 kwa sasa ndio mchezaji anayevuta kisu kirefu kuliko wachezaji in Bundesliga akipata mshahara wa £180,000 kwa wiki.


SCOT PARKER KWENDA WHITE HART LANE BAADA YA KUOMBA UHAMISHO

Scot Parker yupo njiani kujiunga na Spurs muda wowote kutoka sasa baada ya kuomba uhamisho kutoka West Ham United.

Kiungo huyo wa kimataifa wa England aliamua kuingilia kati uhamisho wake baada ya hatihati ya kuvunjika kwa mazungumzo kati Hammers na Spurs kwa kuandika transfer request.

Parker alisema: “Nimekuwa kwa miaka 4 na sitosahau sapoti niliyopewa.Kocha na bodi ya wakurengenzi wajaribu kunishawishi lakini katika stage hii ya career yangu nahitaji kucheza katika premier especially sasa ambapo nina nafasi kwenye timu ya taifa.

Spurs wanategemewa kulipa ada ya uhamisho isiyozidi £6m kumsaini Scot Parker.


PORTO NA CHELSEA WAKUBALIANA ADA YA UHAMISHO WA ALVARO PEREIRA

Star wa Porto Alvaro Pereira yupo njiani kukamilisha ndoto yake kwa kuhamia Stamford Bridge leo.

The Blues jana usiku walikubali kulipa ada ya £20m kwa ajili winga huyo anayecheza kwa pamoja na Luis Suarez kawenye timu ya taifa ya Uruguay.

Raisi wa Porto Pinto Da Costa ameweka wazi kuwa winga huyo aliwekwa nje kwenye mchezo dhidi ya Barcelona ili kumuhepusha na majeraha ambayo yangeweza kuharibu dili la uhamisho kwenda Chelsea.

No comments:

Post a Comment