Search This Blog

Tuesday, August 30, 2011

VALDES AVUNJA REKODI BARCELONA


Victor Valdes sasa ndio golikipa aliyechezea Barcelona mechi nyingi katika historia ya klabu hiyo baada ya kucheza kwenye mechi dhidi ya Villareal na kufanikiwa kufikia rekodi ya kipa wa zamani wa timu hiyo Andoni Zubizarreta ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa michezo wa Barca.

Valdes ambaye alianza kuichezea Barcelona mwaka 2002 na tangu msimu wa 2003/2004 amekuwa hana mpinzani katika milingoti mitatu ya Barca.

Mpaka sasa Valdes ameshalinda lango la Barca katika mechi 410 na amefungwa mabao 323.

Amecheza mechi 296 za La Liga, Champions league 82, 12 spanish cup, 4 Kombe la dunia la klabu, 5 Uefa Cup, 8 Spanish super cup, 3 European Super Cup.

Ameshinda makombe 17, yakiwemo matano ya La Liga, na matatu ya Champions League.

No comments:

Post a Comment