Search This Blog

Sunday, August 14, 2011

Villas Boas aanza kwa sare... Chelsea yashindwa kushinda mchezo wa kumi mfululizo wa mwanzo wa msimu..

Vikosi vilivyoanza .

Tony Pulis aliamua kumpa nafasi ya kuanza Jonathan Woodgate ambaye alikuwa kwenye nafasi yake ya beki wa kati kwenye mfumo usio wa kawaida kwa Stoke wa 4-4-1-1 .

Mfumo huu ni tofauti sana na ule waliotumia msimu uliopita ambapo walikuwa wakichezesha mawinga wawili huku Jonathan Walters akicheza nyuma kidogo ya Kenwyne Jones .
Villas-Boas aliwaacha Drogba na Anelka kwenye benchi akitumia wachezaji wawili pembeni kwenye winga huku Torres akiwa peke yake kama mshambuliaji wa kati .

Chelsea walihangaika sana kukaa sawa kwenye ‘rhythm’ yao na walitumia muda mrefu sana wa kipindi cha kwanza wakihangaika kudeal na mipira ya kurusha ya Rory Delap lakini kadri mchezo ulivyoendelea nao waliendelea ‘kugain momentum’.

Nguvu

Ni moja ya mambo yaliyotarajiwa toka kwa mechi inayowahusisha Stoke ambao wanajulikana kwa kuwa watu wanaotumia nguvu sana kwenye soka lao ambapo tegemeo lao kuu huwa mipira iliyokufa iwe ni ‘free kick’ na mipira ya kurusha .

Stoke City walianza na mabeki wanne wa kati na walitegemea sana mipira iliyokufa na Chelsea kwa upande wao, walijitahidi kuzuia mipira yote iliyokufa ya Stoke City kwa mafanikio makubwa huku kipa Petr Cech akitoka na kupangua mipira yote ya hatari langoni mwake akiwa amezungukwa na msitu wa maadui na mabeki wake .

Mchezo ulikuwa wa tempo yaani spidi ya juu mno tangu mwanzo . Kenwyne Jones na Jon Walters waliwakaba mabeki wa Chelsea karibu kabisa na eneo lao na waliwafanya kina Alex na John Terry wasiwe free kuwachezesha viungo wao wa kati na mara nyingi walilazimika kurudisha mipira kwa golikipa wao, ambaye naye alipiga mpira mirefu mbele mara zote na kumpa wakati mgumu Torres wa kupambana na mabeki wa Stoke.

Jon Walters alikaa sambamba na Jon Obi Mikel ambako alimfanya ashindwe kuiendesha Chelsea kama ilivyo jukumu lake japo Mnigeria huyu aligusa mpira mara nyingi kuliko wachezaji wote kwenye kipindi cha kwanza .
Mstari wa Juu wa Chelsea .

Wakati akiwa na Fc Porto Andre Villas Boas aliwaelekeza wachezaji wake wacheze huku wakikaba kuanzia sehemu ya juu ya uwanja huku mstari wa mabeki ukiwa ngangari na hilo lilionekana hata leo akiwa kwenye mchezo wake wa kwanza na Chelsea, ni kitu ambacho kilionekana kuwanufaisha Chelsea hasa ukizingatia kuwa walimuweka Jones mbali na goli na hivyo hakuwa na madhara huku Terry na Alex wakicheza juu kama maelekezo toka kwa kocha wao yalivyoeleza .
Mbinu hii huwa inaambatana na viungo na washambuliaji nao kukaba tangu wakiwa kwenye nafasi zao lakini bado ilikuwa vigumu sana kutambua mfumo ambao Chelsea ya Andres Villa Boas itakuwa ikicheza .


Mipira ya kipa Asmir Bergovic ilikuwa mirefu na mabeki wa Chelsea muda wote walikuwa wakivuka eneo la kati kumkaba Jones hivyo kulikuwa hakuna nafasi ya ‘kupress’.

Viungo wa Chelsea walishuka chini kidogo na kubana mianya ya mipira hivyo kulikuwa hakuna hatari yoyote toka kwa Stoke .





Wachezaji wa Pembeni.



Mawinga wa Chelsea walikuwa na majukumu tofauti kama unavyoona kwenye mfano wa hapo juu wakitumia mfumo wa 4-3-3.Kwenye maduara meupe ni mawinga ambao walikuwa wanashambulia kwa mtindo wa counter-attack katika mfano ambao hata Jose Mourinho alikuwa akiutumia .






Walianza kwenye nafasi sawa na viungo , baada ya hapo walikimbia na kumsaidia mshambuliaji . Kwenye maduara ya bluu ni mawinga / mabeki ambao walikuwa wakitumiwa ba Carlo Ancelotti wakizuia na pia wakiingia ndani kusaidia viungo na washambuliaji .






Kwenye maduara ya purple ni majukumu ya mawinga chini ya Boas ambapo watakuwa wakikaa eneo la juu la uwanja huku wakiingia kwenye eneo la hatari .



Majukumu ya wachezaji wa pembeni ni moja ya vitu muhimu kwenye soka la Chelsea hasa msimu huu chini ya Andre Villas Boas . Karibu muda wote tangu enzi za Jose Mourinho Chelsea wamekuwa wakitumia mfumo wa 4-3-3 , lakini Mourinho , Ancelotti na Villas-Boas wanahitaji vitu tofauti toka kwa mawinga wao .






Mourinho alikuwa anataka mawinga hasa tena wale wa kizamani ambao ‘wanalala na kuamkia’ pembeni mwa uwanja kama kina Arjen Robben, Shaun Wright-philips na Damien Duff (kidogo na Joe Cole) ambaye alikuwa anarudi mpaka katikati ya uwanja na kufanya Chelsea icheze 4-5-1 wakati timu haina mpira .






Ancelotti kwa upande wake alitumia wachezaji kama Florent Malouda na Nicolas Anelka ambao wanarudi hadi katikati na kuifanya timu icheze kama mfumo wa 4-3-2-1 wakiwa na mpira , mfano mzuri ni wakati Chelsea inatwaa ubingwa wakiifunga United kwa 2-1.



Kwa kutazama muda wake akiwa Fc Porto na jinsi anavyowatumia Malouda na Kalou , Villas Boas anaonekana kuhitaji kiti tofauti . Anataka wachezaji wa mbele ambao wanatopkea kushoto na kuipa timu mabawa halafu wakaingia katikati na kutafuta mabao .






Akiwa Ureno alimtumia Hulk kama mshambuliaji wa Pili kwenye upande wa kulia na Silvestre Valera akiwa anatokea kushoto . Wote wawili wangekaa juu na wangekimbia upande wa pili wa goli pale ambapo mpira ungekuwa kwenye winga .
Haikuwa wazi moja kwa moja ni kitu gani ambacho Kalou na Malouda waliagizwa kufanya . –Kalou alikuwa kimya sana upande wa kulia lakina Malouda alicheza pembeni zaidi kuliko alivyofanya chini ya Ancelotti, japo mara zote utoaji wake wa mipira ulikuwa mbovu pale alipokuwa akipata pasi .
Wakati huo huo Pulis aliwabadilisha mawinga wa Stoke ili kuleta dimension tofauti ya krosi lakini hawakuitisha Chelsea , Stoke walilazimishwa kukimbia mbali na goli . Walichopaswa kufanya ni kuwa na kasi na Walters alishindwa kuipa Stoke Runs muhimu nyuma ya Jones wakati huo huo akimlinda Mikel .







Kipindi Cha Pili .



Chelsea waliongeza kasi na kazi kwenye kipindi cha pili , sababu kuu ikiwa ni presha ndogo ya Stoke mbele ya lango la Chelsea . Pasi za Terry na Mikel zilikuwa na ufasaha na pia kulikuwepo na wakati ambapo Torres alitishia uhai wa Stoke . Combination ya wachezaji wa Chelsea ilikuwa nzuri na wakati Lampard na Ramires walipokimbia kwenda mbele mawinga walionekana kutokuwa na maamuzi mchezoni na wote walitolewa .






Wakati viungo wawili walipopanda mbele, ilikuwa wazi kuwa wachezaji wa Chelsea walifanya over-laps nyingi ili kuwavuta mabeki toka langoni mwao na kumpa mwanya mtu mwenye mpira aingie ndani .






Chelsea walikaribia kufunga kwenye moja ya nafsi walizotengeneza wakicheza hivi ambapo Anelka aligingesha mwamba.
Mpango wa Vilas Boas baadae ulionekana kama umemchanganya hata yeye mwenyewe .






Anelka na Drogba waliingia kwenye nafasi za Kalou na Malouda na Chelsea ikaonekana kama inatumia mfumo wa 4-3-1-2 huku Anelka akiwa nyuma ya washambuliaji wawili , kidogo wakionekana kufanana kimfumo na jinsi Chelsea ya Ancelotti ilivyojaribu kucheza wakati aliposajiliwa Torres.






Mtu ambaye jukumu la Anelka linaonekana kumfaa Yossi Benayoun alipata dakika chache za kuonyesha uwezo wake na ilikuwa pale alipotoka Torres badala ya kuwachezesha pamoja .



Mwisho.



Kuna dalili za mambo mazuri toka kwa Chelsea , ila bado hawajaondoka toka pale walipokuwa msimu uliopita . Wakiwa na kikosi kile kile huku kocha wao akionekana kupendelea mfumo ule ule , mabadiliko machache yatahitajika kidogo , mfano jinsi Chelsea itakavyokuwa ikitumia mpira ndani na wanavyojaribu kuupata mpira pale wanapoupoteza .



Hii ni mechi ya kwanza ngumu kwa Chelsea , na hawakuwa sawa kwa asilimia 100% unazoweza kutarajia toka kwa Chelsea pamoja na kuwa walikuwa wanacheza dhidi ya wapinzani wanaotumia nguvu nyingi .






Hawatalazimika kucheza mchezo ambapompira utakuwa chini kwa muda mfupi zaidi ya ilivyokuwa leo , na Villas Boas anapenda timu inayocheza kwa kushambulia zaidi .
Kwa Stoke hawakuwa tofauti na walivyokuwa msimu uliopita na watafikia malengo yao bila kuhangaika .

No comments:

Post a Comment