Ikicheza kandanda safi lililowavutia wana kampala, Azam FC leo imefanikiwa kuifunga timu ngumu ya Kampala City Council KCC jumla ya magoli 3-0
Azam FC ambayo ipo hapa Kampala ikiendelea na ziara yake ya kujiandaa na ligi kuu ya Vodacom 2011/12 itakayoanza Agosti 20, ilifanikiwa kupata goli la mapema dk 2 ya mchezo kupitia kwa Khamis Mcha Viali
Viali, kinda mwenye umri wa miaka 21 ambaye Azam FC imemnasa kutoka Zanzibar Ocean View alifunga goli hilo baada ya kuwapiga chenga walinzi wawili wa KCC na kumzidi maarifa beki wa pembeni wa KCC aliyekuwa akimsindikiza kasha kumchambua kipa wa KCC na kuujaza mpira ndani ya nyavu.
Baadaye dakika ya ……… Khamis Mcha Viali tena aliwainua vitini mashabiki wachache wa Azam FC baada ya kufunga goli safi kwa mguu wa kushoto kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na John Bocco ambaye alimdondoshea mpira kwa kichwa na viali kumalizia kwa kuuweka ndani ya nyavu.
Baada ya hapo Azam FC iliendelea kutawala mchezo lakini kikosi hicho kilipata dosari baada ya wachezaji wawili wa kimataifa toka nchini Ghana Wahab Yahaya na Nafiu Awudu kuumia na hivyo kutoka na nafasi zao kuchukuliwa na Said Morrad na Zahoro Pazi, na baadaye Kamis Mcha naye alitoka na kumpisha Mrisho Ngasa, Ibrahim Mwaipopo naye alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Jabir Aziz, na John Bocco alitoka na kumpisha Kipre Tchetche.
Ikiwa imesalia dakika moja kabla ya mpira kumalizika, Azam FC ilifanikiwa kupata goli la tatu lililofungwa na Kipre Tchetche ambaye alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Mrisho Khalfani Ngasa.
Katika mechi mbili tatu tulizocheza hapa Kampala Azam FC imeshinda mechi moja, imetoka sare mechi moja na kufungwa mechi moja huku wachezaji Kipre Tchetche na Khamis Mcha Viali wakiongoza kuifungia magoli Azam FC, Khamis Mcha Viali kafunga magoli manne katika mechi mbili alizocheza hapa Kampala huku Kipre akifunga magoli mawili katika mechi Tatu tatu alizoshuka dimbani hapa kampala.
Kesho jioni majira ya saa kumi. Azam FC itashuka kwenye uwanja wa taifa wa Nambole (Mandela Stadium) kukwaana na Victors FC, Victors FC ndiyo timu iliyoifunga Simba 1-0 kwenye tamasha la Simba Day.
Azam FC, Obren, Shikanda, Malika, Aggrey, Nafiu/Morrad, Himid, Ibrahim Mwaipopo/Jabir Aziz, Salum Abubakar, John Bocco/Kipre Tchetche na Khamis Mcha/Mrisho Ngasa
No comments:
Post a Comment