Search This Blog

Wednesday, August 17, 2011

MAELEWANO BAINA YA MABEKI WA KATI WA YANGA NI ISSUE.

sifa kubwa ya Nadir 'Canavarro ' ni kukaba ng'ado kwa ng'ado..

Yanga inajivunia kuwa na mabeki mahili wa kati ambao wanaweza kuwa bora pengine kuliko mabeki wote hivi sasa nchini, Chacha Marwa na Nadir Haroub ‘Canavarro’ . Mabeki hawa wana sifa tofauti zinazoipa Yanga uimara wa uhakika kwenye mstari wa mwisho wa Ulinzi uwanjani .

Nadir Haroub ‘ Canavarro ‘ ni mkabaji mzuri na pia ni mfano halisi wa beki asiyetaka masihara uwanjani . Anajua udhaifu wake wa kushindwa kumiliki mpira na pia hana ‘ball control’ nzuri .

Lakini anajua vyema jinsi ya kuyaziba mapungufu haya kwa umakini wa hali ya juu na maamuzi ya haraka ambayo yamemfanya awe beki bora wa kati nchi Tanzania.Anajua kumbana mshambuliaji na ana nguvu zinazohitajika kwa mchezaji wa nafasi yake .

Chacha Marwa kwa upande wake ni beki mrefu jambo linalomsaidia kucheza vizuri mipira ya juu , ana ujasiri mkubwa anapocheza, jambo linalowafanya washambuliaji wengi kumgwaya wanapopambana naye .

Tatizo kubwa la mabeki hawa wanapocheza pamoja ni kushindwa kuusoma mchezo wa mpinzani na pia kusomana wao wenyewe (hakuna mawasiliano kati yao ) .

Rudisha mawazo nyuma kwenye mchezo wa kwanza wa Kombe la kagame kati ya Yanga na El Mareikh , Nadir Haroub na Chacha Marwa walishindwa kabisa kusoma ‘ movements ‘ za mshambuliaji Jonas Sakuhawa ambaye alipasua katikati yao na kwenda kufunga goli jepesi pasipo bugudha yoyote .


Chacha Marwa hana mbio...kwahiyo ni hatari anapomuachia nafasi mshambuliaji...

Tatizo halikuwa uvivu au ugumu wa watu hawa kukaba kwa kuwa wana uwezo mkubwa sana wa kukaba, tatizo lilikua ni kukosa mawasiliana na kupeana majukumu ya nani atakayekaba na nani atakayesimama,matokeo yake wote walisimama na Mzambia huyu akapenya.

Kosa hili pia lilionekana kwenye mchezo kati ya Yanga na Bunamwaya ambapo Kasule Owen alifunga mabao mawili kwa mtindo huo huo .
Mabeki hawa wanapokutana na mshambuliaji mjanja hali ya wanayanga inakuwa tete kwa kuwa wanashindwa kabisa kukabiliana na mshambuliaji anayetumia akili nyingi na mara zote huwa wanachanganyikiwa wasijue la kufanya.

Kwenye mchezo wa leo dhidi ya Simba iwapo mabeki hawa watapangwa watakutana na kina Gervais Arnold Kago , Felix Sunzu , Emmanuel Okwi na Uhuru Selemani . Washambuliaji wote hawa ni wajanja mno wanaotumia zaidi ‘positioning sense’ na wanapenda kutambaa na mpira yaani wanapendelea zaidi mipira ya chini.

Mabeki wa Yanga kwa upande wao ni wazuri sana kwenye ‘ battles’ yaani mapambano na si wazuri kwenye kukabiliana na washambuliaji wenye kasi na wanaocheza mipira ya chini , hapo Yanga wanaweza kuwa hatarini.

No comments:

Post a Comment