Search This Blog

Wednesday, August 17, 2011

‘MIDFIELD BATTLE’ PATRICK MAFISANGO VS HARUNA NIYONZIMA ‘FABREGAS’.

haruna niyonzima

Moja ya vita muhimu kwenye mchezo wa ngao ya hisani baina ya Simba na Yanga ni mpambano kwenye eneo la katikati ya uwanja kati ya viungo wawili wa kati wa timu hizi mbili ambao wanajuana vilivyo .

Yanga wamemsajili kiungo Haruna Niyonzima ‘Fabregas ‘ ambaye ni mchezaji wa zamani wa APR ya Rwanda . Jina lake la utani ‘Fabregas’ ni ushahidi tosha wa uwezo wa mtu huyu ambaye ametokea kuwa kipenzi cha washabiki wa Yanga .

Hii itakuwa mechi yake ya kwanza ya kiushindani hususani Simba na Yanga na watu wengi watakuwa na hamu ya kuona mchango wake kwenye mechi kubwa .

Kwa upande wa pili Simba wanaye kiungo ambaye kama Fabregas ni raia wa Rwanda na kama Fabregas pia ni mchezaji wa zamani wa klabu ya APR , mtu huyu si mwingine ni Patrick Mutesa Mafisango.

Wakati Mafisango aliposajiliwa na Azam Fc toka APR aliyerithi kitambaa cha unahodha kutoka kwake alikuwa Haruna Niyonzima .

Hii inamaanisha kuwa wachezaji hawa wawili walikuwa wachezaji muhimu kwenye timu yao , yaani kama Fabregas alikuwa namba moja basi aliyefuatia alikuwa Mafisango au kinyume chake yaani kama Mafisango alikuwa bora basi Fabregas alikuwa anafuatia nyuma yake , umuhimu wao kwa timu ulikuwa kama ilivyo kwa Roho na Moyo kwenye mwili wa mwanadamu kama ilivyo kwa Liverpool wanaposema ‘Gerard is the Soul of the Team and Caragher is the Heart of the team’.


Watu hawa wote ni viungo wa kati na japo walikuwa wanacheza timu moja katika nafasi tofauti wamejikuta wakiwa kwenye eneo moja kwenye timu tofauti .

Kwa mechi chache alizocheza Mafisango kwenye timu ya Simba wakati wa kombe la kagame ameweza kuteka hisia za mashaii wa timu yake kwa uwezo wake mkubwa aliounyesha .

Ana ‘ball control’ ya kiwango cha juu , ana akili za ziada na aliipa uhai safu ya kiungo ya Simba ambayo imeonekana kupwaya sana kwa siku za nyumas kabla ya ujio wake .

Usajili wa Niyonzima umekuwa gumzo nchi nzima na ukijudge kwa mapokezi aliyopewa na wanayanga wakati anakuja toka Rwanda kukamilisha mchakato wa kusajili utaona kuwa wanayanga wamemuweka kiungo huyo sehemu gani kwenye mioyo yao .

Wachezaji hawa wanaojuana sana kutokana na kuwa pamoja kwa miaka mingi kwenye klabu moja na kwenye timu moja ya taifa kutafanya pambano la Simba na Yanga kwenye ngao ya hisani kuwa la aina yake hasa ukizingatia ‘battle’ ngumu itayokuwepo baina yao kwani kila mmoja natarajiwa kuwa dereva wa timu yake kwenye eneo la kiungo .

Mafisango ana urefu ambao unampa faida kubwa juu ya mwenzie ambaye ni mfupi , lakini Fabregas kwa ufupi wake anakuwa na akili nyingi za ziada ambazo mara nyingi wachezaji wafupi wanakuwa nazo na pia ‘low centre of gravity’ aliyo nayo fabregas kutokana na ufupi wake ni faida kubwa kwake .

Je ni nani kati ya viungo hawa wawili toka taifa moja na klabu moja pia atayeondoka uwanjani akiwa na furaha kuliko mwenzie ? Jibu litapatikana baada ya kipenga cha mwisho.

No comments:

Post a Comment