Search This Blog

Wednesday, August 17, 2011

MWAPE,ASAMOAH,KIIZA VS KAGO,SUNZU,OKWI.

Ukosefu wa washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa kufumania nyavu hapa nchini Tanzania umesababisha timu kubwa za Simba na Yanga kuvuka mipaka , milima na mabonde kwenda kutafuta washambualiaji kwenye nchini nyingine.
Yanga wana safu ya washambuliaji ambayo ina nchi tatu tofauti Uganda,Zambia na Ghana .


Washambuliaji wanaotoka kwenye nchi hizo ni Davis Mwape - Zambia , Hamis Kiiza -Uganda japo ana chembechembe za asili y Tanzania na Keneth Asamoah-Ghana alipeleka kilio msimbazi mara ya mwisho kwa bao lake safi lililoipa ubingwa wa Kombe la Kagame timu yake .

Kwa upande wa Simba safu yake ya ushambuliaji ina kina Felix Mumba Sunzu -Zambia,Emmanuel Okwi - Uganda na Gervais Arnold Kago - Jamhuri ya Afrika ya kati .

Washambuliaji hawa wote kwa nyakati tofauti wameonyesha uwezo mkubwa ambao umewafanya viongozi wa timu hizi mbili kupigana kufa na kupona kuwasajili na kuwapa huduma nzuri ili mradi tu waendelee kuwepo kwenye timu hizo .
Davis Mwape ni mshambuliaji mwenye uwezo na uzoefu mkubwa . Amewahi kuichezea klabu kubwa ya Orlando Pirates kwenye ligi ya PSL nchini Afrika Kusini na ujio wake kwenye klabu ya Yanga msimu uliopita ulikuwa wa mafanikio kwani kwenye mechi chache alizocheza kwenye ligi kuu ya Vodacom aliweza kufunga mabao 6 .


Hamis Kiiza naye ni mfungaji hodari wa mabao . Kwa wale waliokuwa wanafuatilia maendeleo ya timu ya taifa yak vijana wenye umri chini yak miaka 23 watamkumbuka vizuri Kiiza kwani alifunga mabao muhimu yaliyoitoa timu ya vijana na shughuli hiyo hiyo aliihamishia kwenye mchezo dhidi yak timu ya vijana ya Kenya ambapo jijini Nairobi alifunga ‘hat-trick ‘ .

Hakuishia hapo kwenye michuano ya kombe la kagame alifunga mabao mawili huku akitoa mchango mkubwa kwa timu yake kwa kujituma vilivyo kwenye mchezo wa fainali dhidi ya wapinzania wao wa jadi Simba .

Bila shaka anaingia moja kwa moja kwenye orodha ya wachezaji muhimu watakaopewa kipaumbele kwenye kikosi cha kwanza cha yanga ingawa amekuwa na matatizo na uongozi kwa siku za karibuni.






Keneth Asamoah ametokea kuwa mshambuliaji muhimu kwa timu yake tangu alipoichezea Yanga kwa mara kwanza kwenye michauno ya Kagame .
Asamoah aliingia kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Al Mareikh akichukua nafasi ya Jerryson Tegete na alimtia presha beki wa Al Mareikh na kumfanya ajifunge na kuipa timu yake bao muhimu.




Asamoah aliingia moja kwa moja kwenye mioyo ya wapenzi wa Yanga kwa bao lake aliloifunga Simba kwenye fainali na rekodi yake nzuri dhidi ya Simba itampa nafasi kwenye mchezo dhdi ya Simba.




Emanuel Okwi ni mmoja wa washambuliaji muhimu walioko kwenye timu ya Simba .




Uwezo wake wa kuwachukua mabeki wa timu pinzani kwa chenga zake na uwezo wa kumiliki mpira mguuni ni jambo ambalo siku zote limewapa tabu wapinzani wake anapokuwa uwanjani , kama kuna mtu ambaye uwepo wake unawapa wanasimba imani basi ni okwi, na wengi wao ukiwauliza watakwambia kuwa mara ya mwisho Simba walifungwa kwa kuwa Okwi hakuwepo .

Felix Sunzu , Mengi yamezungumzwa kuhusu Mzambia huyu . Amewahi kucheza dhidi ya Yanga akiiwakilisha klabu ya Fc Lupopo na uwezo wake mkubwa wa kuwafungasha tela mabeki wa Yanga siku hiyo ulidhihirika na Simba wamemtafuta tangu wakati huo .




Alikuwa moja ya sababu za wanayanga kumchukia beki wao Mmalawi Wisdom Ndlovu kwani walimtupia lawama za kumwachia Sunzu kirahisi. Alikuja nchini wakati wa Kombe la Challenge na kwa mara nyingine alionyesha uwezo wake kwa kufunga mabao manne , baadaye alisajiliwa na AL Hilal ila mambo hayakumwendea vyema kwani katika miezi sita aliyokaa Sudan hakufunga bao hata moja .




Ameonyesha uhai mkubwa kwenye mechi za majaribio za Simba na amekuwa mshambuliaji tegemeo kwenye timu hiyo.




Gervais Arnold Kago. Mshambuliaji huyu ametokea kuwa gumzo katika vinywa vya wadau wa soka hivi karibuni . Shirikisho la TFF lilimuwekea ngumu kucheza kwenye mchezo wa ngao ya hisani lakini baadae shirikisho hili lilirudi nyuma na kumruhusu acheze .




Uwezo wake ni mkubwa japo si wengi wanaomfahamu ila kwa wale waliofuatilia mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kati ya Taifa Stars na Jamhuri ya Afrika ya kati watakubali kuwa huyu jamaa ni hatari.




Alimtungua kipa wa Stars siku hiyo Shaban Kado kwa shuti moja la nguvu kwenye ‘imposible angle’ , alirudia kitu hicho kwenye mchezo uliofanyika jijini Bangui na ni mechi hizo mbili ndio zilizowapa viongozi wa Simba sababu ya kumsajili .Tegemea mengi na makubwa kutoka kwake .

No comments:

Post a Comment