Search This Blog

Friday, August 19, 2011

DEIN: KUWENI NA HESHIMA KWA WENGER AU ATAONDOKA


Arsene Wenger anaweza kuacha kazi ya ukocha Arsenal ikiwa mashabiki wataendelea kuwakosea adabu yeye na kikosi chake, makamu mwenyekiti wa zamani wa Gunners David Dein amesema.

Akiongea na shirika la habari la Uingereza, alionya kuwa kocha huyo mfaransa yupo njia njiapanda, huku mashabiki wakiendelea kuonyesha hasira zao juu ya Arsenal kukosa ubingwa kwa miaka 6 mfufulizo.

Dein alisema kuondoka Emirates inaweza ikawa chaguo kwa Wenger kwa sababu itafikia kipindi atasema “Imetosha”.

“Hivyo mimi ndivyo ninavyoona na ni vizuri na mashabiki wakawa na mtazamo huo, wanatakiwa atleast kumpa heshima anayostahili kwa mambo mazuri na makubwa aliyoifanyia klabu hii,

“Watu wanazungumza kuisha kwa muda wake kuwepo klabu kuisha?

“Hilo ni jambo la hatari kuzungumza kwa sababu ni rahisi kuwatimua watu kazi halafu nini kinafuata?Watu wanaongea kuhusu kununua wachezaji wapya.Sawa lakini hilo linaweza lisiwe suluhisho,

“Naelewa wasiwasi wa mashabiki , lakini Arsene Wenger amekuwa nasi kwa zaidi ya miaka 15 na kila msimu tumekuwa tukifaulu kucheza ligi ya mabingwa, ingawa mashabiki bado wana hamu ya kushinda kombe.

“Chini ya uongozi wa Arsene Wenger tumekuwa na vipindi vingi vya furaha na naamini hakuna sababu itakayotufanya tusiwe tena na furaha tuliyowahi kuwa nayo.”

No comments:

Post a Comment