Search This Blog

Friday, August 19, 2011

PROFESSOR JAY: MIMI NI MSIMBAZI DAMU


Siku ya Jumatano tarehe 17, August, ilikuwa ni siku nzuri sana kwa mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania Joseph Haule a.k.a Professor Jay, baada ya timu yake ya soka anayoishabikia kuifunga timu pinzani.

Professor Jay ambaye ni mnazi na shabiki mkubwa wa Simba Sports Club, watoto wa Msimbazi, anasema alianza kuipenda Simba tangu alipopata ufahamu wa soka mpaka sasa amekuwa mpenzi mkubwa klabu hiyo ndio maana siku ya Jumatano iliyopita ilikuwa siku ya furaha baada ya Mnyama kumuumiza Yanga 2-0 katika mchezo wa Ngao ya Hisani.

“Mimi shabiki wa kutupwa wa Mnyama kiasi kwamba tukifungwa nakosa sana amani na furaha kwa siku nzima, na kama ilivyo kawaida timu ambayo sina kabisa mapenzi nayo hapa Bongo ni mtani wetu wa Jadi Yeboyebo “Dar Young African”.


“Kwa upande wa nje ya Bongo, kwanza siipendi kabisa Manchester United kwa kuwa mimi ni Liverpool damu, yaani huniambii kitu kuhusu The Reds.Huu ndio muda wetu wa kurudisha heshima yetu iliyopotea kwa kipindi kirefu, kwa sababu timu chini ya King Kenny Daglish imefanya usajili mzuri sana.Watu kama Luis Suarez, Stewart Downing, Charlie Adam na wengineo watatusaidia sana.Man U na timu nyingine wajitaarishe kwa vipigo tu msimu huu na kazi inaanzia kwa Arsenal kesho, na wengine waelekee Qibra mapema tukija tunachinja tu.

Liverpool “we will never walk alone”. – Prof.Jay

1 comment:

  1. duh! Me ni shabiki wa kutupwa wa prof. Ila sikuwah kujua kama tuna share in common ushabiki wa soka,lykwise prof j,naipenda sana sana SIMBA na LIVERPOOL! Duh hii imeniongezea ushabiki kwa prof asee!duh! Me ni shabiki wa kutupwa wa prof. Ila sikuwah kujua kama tuna share in common ushabiki wa soka,lykwise prof j,naipenda sana sana SIMBA na LIVERPOOL! Duh hii imeniongezea ushabiki kwa prof asee! naitwa Dickson Joseph kutoka Musoma

    ReplyDelete