Search This Blog

Thursday, July 21, 2011

ULIKUWA NI UAMUZI RAHISI KUICHAGUA UNITED - ASHLEY YOUNG


Ashley Young alikuwa tayari ameshaichagua Man United mara tu baada ya kujua wanamuhitaji.

Huku mkataba wake na Aston Villa ukiwa unakaribia kuisha mwishoni mwa msimu uliopita, ni wazi ilijulikana kuwa ataondoka Villa Park.

Young, 26, anasema alikuwa ameshafanya maamuzi kuhusu future yake, na ilikuwa ni suala la kuthibitisha tu uhamisho wake kuelekea Old Trafford kwa paundi million 17..

"Sikuwahi kuwa na mashaka pindi tu nilipojua United walikuwa wakinitaka, pindi moja ya klabu kubwa duniani inapokufuata si rahisi kukataa.Nilikuwa na furaha kusikia kuhusu wao kuvutiwa na mimi, na nilikuwa nasubiri kuweka saini yangu kwenye vitabu."

Mchezaji huyu wa kimataifa wa England pia anasema ana uhakika atafanikiwa akiwa na jezi ya United: "Ninajiamini kutokana na uwezo wangu, siku zote nimekuwa nikitaka kucheza katika level ya juu, na Mancheter United ni mahali sahihi.Uhamisho huu umenipa nafasi ya kucheza katika ligi ya mabingwa na pia kuisadia timu yangu kushinda ubingwa wa 20 wa ligi.Nataka kuwa moja ya sehemu ya timu ya ushindi.Kutokea siku ya kwanza nilipowasili, kocha amekuwa akiongea kuhusu kuwa na mentality ya ushindi.Unaweza ukaona matamanio ya ushindi hata ukiwa mazoezini, hii klabu ni kila kitu kuhusu ushindi." -YOUNG


No comments:

Post a Comment