Search This Blog

Thursday, July 21, 2011

DAKIKA 14 ZA NGASSA DHIDI YA MAN UTD.

Mpambano uliokuwa unasubiliwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka ulimwenguni kati ya Seattle Sounders na Manchester Utd umemalizika kwa Man Utd kufanikiwa kuichapa Sounders Mabao 7-0.
Man Utd wapo kwenye Tour ya Marekani kujiandaa na msimu mpya wa 2011/12 huku Sounders wakiwa na msimu mzuri sana wa MLS kwani ni moja kati ya timu zinazofanya vizuri kwenye ligi hiyo.
Kabla ya mchezo baina ya hizi timu mbili mashabiki wa Sounders walikuwa na matumaini ya kuifunga Man utd lakini walisahau ya kwamba pamoja na timu yao kuwa na matokeo mazuri kwenye MLS bado walikuwa na rekodi mbaya kwenye safu yao ya ulinzi.
Kabla ya mchezo dhidi ya Man utd, Sounders ilikuwa imecheza jumla ya michezo 24 na kati ya michezo yote hiyo ni michezo mitano waliyomaliza pasipo kuruhusu wavu wao kuguswa, na cha kustaajabisha wamefungwa jumla ya mabao 25 ,wastani wa bao moja kwa kila mchezo,safu yake ya ushambuliaji ikiongozwa na Fredy Montero pamoja na Mauro Rosales ndiyo imekuwa ikiibeba timu hiyo, kwa aina ya mchezo wanaocheza wa kushambulia tu haishangazi kutandikwa 7-0 na Man utd,
Man utd walianza na Luis Nani na Ashley Young kwenye wingi zote mbili,huku Anderson na Ryan Giggs wakiificha mipira yote katikati na matokeo yake Sounders wakalazimika kuingia msituni kuutafuta mpira kitu ambacho lilikua ni kosa la jinai, Ashley Young na EVRA walikua wanampiga ‘mande ‘ beki wa kulia wa Sounders , ‘the Douglas Maicon’ wa MLS James Riley. Upande wake wa kulia ndo ulikua chimbuko la bao la kwanza lilifungwa na Michael Owen kwa kichwa huru,
Pia tusisahau kuwa level ya man utd huwezi kuilinganisha na Seattle Sounders kutokana na utofauti wa ligi wanazocheza.
Nimesoma comments kadhaa za mashabiki wa soka nchini Tanzania Wengi wanadhani Mrisho Ngassa alikuwa muoga kwa mabeki wa Man utd,kitu ambacho binafsi nakipinga tena kwa nguvu zote,
Kiukweli timu nzima ya Seattle ilikuwa inaihofia Man Utd na kama wangekuwa makini kuzitumia nafasi kadhaa walizozipata sidhani kama ubao wa matokeo ungesomeka vile, takwimu tu zinaweza kukupa jibu,.kwenye mchezo huo Sounders walipiga jumla ya mashuti 18 golini mwa Man Utd huku mshambuliaji wao nyota Fredy Montero akipiga mashuti 5 peke yake pasipokufunga walau goli moja,
Wakati Man Utd walipiga jumla ya mashuti 20 golini wakapata mabao 7 huku Wayne Rooney akipiga jumla ya mashuti 4 na mashuti matatu akaweka mpira kambani.
Kipindi cha pili Man utd walimwingiza Wayne Rooney ambaye hakuchelewa kutumia mianya mingi iliyokua inajitokeza kwenye lango la Sounders na kufunga jumla ya mabao matatu.
Usitegemee unapocheza na timu imara kama Man Utd na ukaipa uhuru wa kutengeneza nafasi nyingi itakuacha.

Dakika 14 za MRISHO NGASSA
Binafsi nimefurahishwa na namna Ngassa alivyocheza, Sounders wanamtafuta mbadala wa winga wao Steve Zakuani aliyepata majeraha ya muda mrefu,
Moja kati ya sifa za mchezaji wa kuziba nafasi ya Zikuani anatakiwa awe na spidi, awe na movements nzuri akiwa au hana mpira, moja kati ya vitu vilivyonifurahisha kwa Ngassa ni hali ya kujiamini aliyokua nayo,tukumbuke kwanza Ngassa hakuwa mchezaji wa Sounders bali alipewa nafasi ili wampime uwezo wake kwenye mechi kubwa kama dhidi ya Man Utd,
Nilipata wasaha wa kufanya mahojiano na mkurugenzi wa ufundi wa SONDERS bwana Chris Henderson binafsi alivutiwa sana kipaji cha Ngassa.

Ngassa Kukosa nafasi ya wazi....
Narudia tena tusiangalie tu kupoteza nafasi ya kufunga,ni muhim pia kuangalia namna hiyo nafasi ilivyotengenezwapia ,tuangalie mazingira ya namna alivyoipata ile nafasi ya kufunga lile bao,mi nadhani cha msingi tuangalie alikimbia umbali kiasi gani kuufikia ule mpira na Rio Ferdinand alikuwa umbali kiasi gani na ule mpira, tukiangalia hivyo vitu nadhani tutapata picha kabla ya kulaumu.


No comments:

Post a Comment