Search This Blog

Friday, July 22, 2011

DC MOTEMA PEMBE MBIONI KUMSAJILI MGOSI


Daring Club Motema Pembe (DCMP) ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kupitia Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu vya nchi hiyo (FECOFA) limetuma TFF maombi ya Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mshambuliaji wa Simba, Musa Hassan Mgosi. Klabu hiyo imemuombea Mgosi hati hiyo ya uhamisho kama mchezaji wa ridhaa kwa maelezo kuwa imeshakubaliana na wenzao wa Simba katika suala hilo. Hivyo hivi sasa TFF inafanya mawasiliano na Simba kabla ya kufikia uamuzi wa kutoa ITC kwa DCMP.

No comments:

Post a Comment