Search This Blog

Friday, July 22, 2011

OFFICIAL: SANCHEZ AJIUNGA NA BARCELONA


Hatimaye klabu ya Barcelona imefanikiwa kuzishinda klabu za Man UTD, City, na Chelsea baada ya leo kufanikiwa kumsajili winga wa kimataifa wa Chile Alexis Sanchez kwa gharama ya £22million (Add ons £11m).
Sanchez ambaye amekuwa moja ya wachezaji waliokuwa wakihusishwa kwa kiasi kikubwa na mabingwa wa ulaya anatarajiwa kwenda nchini Spain Jumatatu ijayo kufanyiwa vipimo na baadae majibu ya vipimo yakiwa postive mchezaji huyo atasaini mkataba wa miaka 5 wa kuitumikia klabu hiyo.
Kupitia mtandao rasmi wa klabu hiyo walitoa taarifa isemayo: "Udinese and F.C Barcelona wamekubaliana juu ya uhamisho wa Alexis Sanchez.Vipimo, kusaini mkataba wa miaka 5 na kutambulishwa kutafanyika Jumatatu."

No comments:

Post a Comment