Search This Blog

Saturday, July 23, 2011

NASRI AKATAA MSHAHARA WA £115,000 ATISHIA KUONDOKA BURE


Samir Nasri yupo radhi kubaki Arsenal msimu huu na kuondoka bure msimu ujao.
Kiungo huyo wa kifaransa amewaambia wachezaji wenzie kuwa hatosaini mkataba mpya na Gunners, atakataa dili la mshahara wa £115,000 kwa wiki huku akiwa matumaini ya kulazimisha uhamisho wa kwenda Manchester City.
Nasri, ambaye aliondoka na kikosi cha Arsenal kwenda Ujrumani kucheza mechi ya kirafiki na FC Cologne, amewaambia wachezaji wenzie kuwa anaweza kubaki Emirates msimu huu na kuondoka bure next summer.
Jana, Arsena Wenger alipoulizwa kuhusu hatma ya Nasri alisema: "Makubaliano bado hajakamilika, lakini nataka abaki na yeye anajua.Naamini suala hili litamalizika ndani wiki chache zijazo."
Wakiwa kwenye ziara nchini Malaysia Wenger alipoulizwa alisema anataka Nasri na Fabregas waendelee kubaki lakini mara tu Gunners walipompa mkataba wa £115,000 Nasri alikataa kwa haraka sana.

No comments:

Post a Comment