Search This Blog

Friday, July 22, 2011

MAMBO 5 ALIYOJIFUNZA MRISHO NGASSA AKIWA NA SEATTLE SOUNDERS.

1. KUHESHIMU MUDA.

Moja kati ya vitu muhimu nilivyojifunza hapa ni kuheshimu muda

hapa, jamaa wanafuata sana ratiba iliyowekwa kabla na baada ya mazoezi,

mfano saa moja kabla ya muda wa mazoezi kila mchezaji anatakiwa kuwa ameshafika uwanjani, nusu saa kabla umeshavaa vifaa vya mazoezi,dakika 20 kabla upo uwanjani unafanya mazoezi binafsi.

2. KULA KABLA YA KUANZA MAZOEZI NI KITU MUHIMU MNO.

Aisee unaweza ukaona ni kitu cha kawaida lakini nimegundua kwanini makocha wa kigeni wanasisitiza kula kabla ya mazoezi kuanza, siyo ukisikia kula ni kwenda tu kunywa kikombe kimoja cha chai na andazi moja,hapana unakula msosi wa haja maana mazoezi yanakua magumu sana na yanahitaji uwe umeshiba kweli.

3. UKISIKIA BENCHI LA UFUNDI NI LA UFUNDI KWELI.

Hawa jamaa hawana utani hata kidogo,kwanza kwenye utawala wa timu kuna watu wengi kushinda hata idadi ya wachezaji wakati wa mazoezi,

kuna watu maalum kwa ajili ya kufundisha mfumo wa namna gani timu inatakiwa kucheza kwa njakati tofauti tofauti,mfano timu inatakiwa ichezeje ikiwa inataka iwe ya kwanza kufunga bao,na hata ikitokea timu imeanza kufungwa kitu gani kinatakiwa kufanyika ndani ya muda mfupi cha kubadilisha mfumo wa uchezaji.

kuna watu kazi yao ni kudili na majukumu mbali mbali mfano, magolikipa,washambuliaji,mabeki,viungo, nk

yaani benchi la ufundi lina watu wengi sana kushinda unavyoweza kuzania.

4.HAKUNA MAMBO YA KAMBI HUKU

mimi tangia nimefika huku hakuna mtu wa kunifuatilia eti nafanya nini,nilipofika hapa nikapewa nyumba ya kuishi,baada ya hapo nikapewa ratiba ya mazoezi,kilichobaki jamaa walikua wananiletea usafiri wa kunipeleka na kunirudisha nyumbani,

huku siyo kama nyumbani eti kambi kwanza hata mimi sioni ulazima wa mambo ya kambi hayamfanyi mchezaji kuwa katika hali ya kujipangilia mambo yake ya kimaisha na kazi.

huwezi amini hata siku ya mchezo wetu dhidi ya Man utd kila mchezaji alifika uwanjani na usafiri wake,cha muhim kilikuwa ni kufika uwanjani lisaa limoja kabla ya mchezo kuanza.

5. MUDA WA MAZOEZI SI CHINI YA MASAA 4 KWA SIKU.

huku hakuna cha kufanya mazoezi ya Asubuhi na Jioni, mazoezi yanafanyika asubuhi tu na baada ya hapo kila mchezaji anaenda zake nyumbani,lakini ukifika nyumbani siyo unalala,unatakiwa ufanye gym,upumzike na ule kweli kweli.












No comments:

Post a Comment