Search This Blog

Friday, July 22, 2011

MODRIC ANA THAMANI ZAIDI YA £35MILLION


Kocha wa Tottenham Harry Redknapp amesisitiza kuwa mchezaji wake Luka Modric ana gharama ya zaidi ya £35million.
Modric ambaye amesema wazi kuwa anahitaji kuondoka White Hart Lane amekuwa akisakwa kwa udi na uvumba na matajiri wa London, Chelsea ambao tayari walishatuma ofa ya £22million na baadae wakaongeza mpaka £27m.
Akizungumza na Press Redknapp alisema: "Kama tungekuwa tumeamua kumuuza basi hata £35m haitokuwa sahihi kwa Luka, ana thamani ya pesa nyingi zaidi.
Kiukweli hatutaki kumuuza Modric, tunahitaji kuendelea kuwa na wachezaji wetu bora.Uamuzi wa kuuza mchezaji wa mwenyekiti Levy, lakini mimi kama kocha nisingependa kuondokewa na mchezaji kama Luka."

No comments:

Post a Comment