Search This Blog

Thursday, June 9, 2011

TURKEY FA - TUTAWASHTAKI FIFA CHELSEA


Shirikisho la soka la Uturuki limewaonyaChelsea kuwa watatshatakiwa kwa FIFA ikiwa watajaribu kumshawishi isivyo halali Guus Hiddink kujiunga nao.

Inaeleweka kuwa mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anajiandaa kumrudisha kocha huyo wa kiholanzi Stamford Bridge sehemu ambayo Hiddink alifanya kazi kama kocha wa muda wa klabu hiyo mwaka 2009.

Lakini kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 ana mkataba wa kuifundisha timu ya taifa ya Uturuki mpaka mwakani na sasa shirikisho la soka la Uturuki limeionya klabu hiyo kuwa litawashtaki kwa FIFA ikiwa watajaribu kupitia mlango wa nyuma na kumshawishi Guus kujiunga nao akiwa bado na mkataba na TFF.


"Chelsea wana tabia ya kuwasajili wachezaji walio ndani ya mikataba, kama kitu kama hichi kikitokea kwa Hiddink tutawashtaki kwa FIFA.Waheshimu mkataba ambao Guus na FA." alisema Raisi wa TFF Mahmut Ozgener alipoongea na gazeti la Uturuki la HURRIYET..



No comments:

Post a Comment