Search This Blog

Thursday, June 9, 2011

MFUKO WA BARCA HAUTOSHI KWA FABREGAS


Mpango wa Barcelona kumchukua Cesc Fabregas kutoka Arsenal unaonekana upo mashakani baada ya Catalunya club kutangaza bujeti yao ya uhamisho kuwa ni £40, kiasi ambacho ni pungufu ya £10 ya gharama ya kumsajili kiungo huyo kutoka Emirates.

Barca wamechukua hatua isiyo ya kawaida kutangaza bajeti ya uhamisho baada kuthibitisha kuwa wanachukua hatua za kupunguza deni la klabu.

Makamu wa Raisi wa kitengo cha masuala ya pesa wa mabingwa hao wa ulaya Javier Faus alisema, "Pep Guardiola atapata £40million kwa ajili ya kusajili kwa pamoja na pesa itakayopatikana kupitia mauzo ya wachezaji

Kiasi hiki ni kidogo tofauti na Arsenal wanavyotaka kwa ajili ya Fabregas ingawa kinaweza kupanda ikiwa Barca watawauza Bojan Krkic, Jeffren na Maxwell.


No comments:

Post a Comment