Search This Blog

Thursday, June 9, 2011

Ada ya paundi milioni 30 kumpeleka alexis Sanchez Old Trafford.

Manchester United ipo mbioni kutumia kiasi paundi milioni 30 ( £30million) kwa ajili ya kupata saini ya winga Alexis Sanchez kutoka Udinese.
United walikua wanafikilia kumpata winga huyo raia wa Chile mwenye umri wa miaka 22, kwa kiasi cha paundi milioni 25 – lakini klabu yake imegoma kutoa apunguzo la ada yake ya uhamisho.
Sanchez mwenyewe anataka kujiunga na vijana wa Alex Ferguson kuliko Barcelona, akijua fika atatumia muda mrefu kuchoma mahindi pale Nou Camp.wakala wake, Fernando Felicevich, amedhibitisha kukutana na na mabosi wa barcelona lakini akadhibitisha pia hakuna dili lolote lililofanyika. Pia akasema ana matumaini makubwa iwapo udinese na Manchester Utd watakubaliana ada ya uhamisho basi Sanchez atajiunga na Man utd muda wowote.

No comments:

Post a Comment