Search This Blog

Saturday, June 18, 2011

Timu ya U23 imewasili salama nchini Nigeria

THOMAS ULIMWENGU ATAONGOZA SAFU YA USHAMBULIAJI.

Boniface Wambura, Lagos

Timu ya U23 imewasili salama hapa saa 6.30 mchana kwa ndege ya Kenya Airways
kabla ya kuunganisha ndege ya Concord Airlines kwenda Benin City ambapo mechi
dhidi ya Nigeria itachezwa kesho kuanzia saa 10 kamili saa za hapa ambapo
nyumbani Tanzania itakuwa saa 12 kamili jioni.

Awali U23 ilikuwa ifike hapa saa 4 kamili asubuhi, lakini ikachelewa kutoka
Nairobi ambapo ilitoka saa 3.30 badala ya saa 1.30 baada ya ndege ya Kenya
Airways kuchelewa kuondoka.

Kocha Jamhuri Kihwelo amesema vijana wake katika hali nzuri ya kupeperusha
bendera ya Tanzania katika mechi hiyo ambapo mshindi baada ya matokeo ya
nyumbani ambapo U23 ilipata ushindi wa bao moja ataingia katika hatua ya makundi
kutafuta tiketi ya kuiwakilisha Afrika katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika
mwakani jijini London, Uingereza.

Amesema timu yake itacheza mchezo wa kushambulia kwa kushtukiza huku akijaza
viungo wengi kwa lengo la kumiliki mpira kwa muda mrefu, hivyo kuzuia
mashambulizi ya timu pinzani kwa staili.

Kihwelo amesema mbele atatumia washambuliaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata.
Wachezaji wengine aliokuja nao hapa ni Jamal Mnyate, Jackson Wandwi, Hussein
Javu, Mohamed Soud, Obadia Mungusa, Abuu Ubwa, Juma Abdul, Abdul Juma, Himid
Mao, Issa Rashid, Khamis Mcha, Salum Abubakar, Shomari Kapombe, Jabir Aziz,
Godfrey Wambura na Awadh Juma.

No comments:

Post a Comment