Search This Blog

Saturday, June 18, 2011

NATAKA KUONDOKA - MODRIC


Luka Modric amewashangaza mashabiki wa Tottenham baada ya kukiri anataka kuondoka White Hart Lane.

Modric mwenyewe amevunja kuhusu suala la usajili wake baada kusema nataka kuondoka Spurs.

Akiongea na gazeti la Daily Mail, alisema: "Nataka kuondoka Tottenham nikiwa na uhusiano mzuri na klabu, nilifurahia sana uwepo wangu pale lakini huu ni muda sahihi kwangu kuangalia klabu nyingine."

Nimekuwa na makubaliano na mwenyekiti.Nilipokuwa nasaini mkataba alianiambia, ikitokea klabu itakayonitaka wataifikiria ofa.

Modric ambaye Chelsea juzi walipeleka ofa rasmi kwa Spurs na amekuwa akiuhusishwa pia na kujiunga na United lakini inaonekana Chelsea wana nafasi kubwa zaidi.

"Chelsea ni klabu kubwa na ina mmiliki mwenye ndoto za kufanikiwa.Wana wachezaji wazuri na wenye hamu ya mafanikio kwa kupigana kushinda EPL na Champions League.

"Nataka kubaki London.Nina furaha ndani jiji hili na pia familia yangu wanapapenda hapa."


No comments:

Post a Comment