Search This Blog

Thursday, June 9, 2011

NIPE NAMBA AU NAONDOKA - KUSZCZAK AMWAMBIA FERGIE


Tomasz Kuszczak ametishia kuhama Manchester United ikiwa hatakuwa golikipa namba moja Old Trafford.

The 29-year old Polish goalkeeper amekuwa akikaa benchi kwa zaidi ya miaka minne na sasa Van Der Sar amestaafu Kuszczack anaona ndio muda muafaka wa kupata nafasi.

Lakini kutokana na taarifa za ujio wa kipa David De Gea kutoka Atletico Madrid, Kuszczack amesema wazi kuwa anataka kucheza au aondoke.

"Kwangu mimi ipo wazi kabisa nicheze kwenye goli la United au niondoke hapa", aliiambia France Football.

“Sir Alex Ferguson hajaniambia chochote kuhusu mkataba mpya.Hajaniambia chochote ,sijui nifikirie nini.Nina mawazo fulani hivyo nitajua cha kufanya.Nafikiri nitaendelea kubaki England nimekuwa pale kwa miaka saba, na uwezo wangu unafahamika pale.".

No comments:

Post a Comment