Search This Blog

Monday, June 6, 2011

BAADA YA CHICHARITO SASA ERICK TORRES


Maaskauti wa kutafuta vipaji wa klabu ya Manchester United leo wapo jijini Toulon-France kumfuatilia mchezaji wa timu ya Chivas Erick Torres. Torres ambaye pia nae ni raia wa Mexico leo atakuwa uwanjani wakati timu yake ya Mexico itakapokuwa ikicheza na China. Man United wameonekana kuvutia na Torres ambaye amefunga magoli sita katika michezo 19 tangu aanza kuichezea Chivas in November kama mrithi wa Javier Hernandez Chicharito. Erick Torres kwa sasa yupo kwenye kikosi cha Mexico under 20 kwa ajili ya mashindano Toulon yanayofanyika Ufaransa.

PSV Eindhoven nao wameonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo, lakini wana nafasi nzuri hasa zaidi baada ya kuwa uhusiano wa karibu na Chivas baada ya kumsaini Chicharito kwa paundi million 6 mwezi 4 mwaka jana, Sir Alex Ferguson na Chief Scouter Jim Lawlor tayari wameshavutiwa na uwezo wa Torres.

No comments:

Post a Comment