Search This Blog

Sunday, June 5, 2011

ARSHAVIN - FABREGAS AMETUAGA


Andrey Arshavin anahofu kuwa Cesc Fabregas anaondoka Arsenal baada ya kiungo wa Hispania kuwapa zawadi za kuagana na wachezaji wenzake wa Gunners.
Fabregas ambaye mwaka jana aliomba kuuzwa Barcelona lakini ikashindikana amekuwa ni hot cake katika soko la uhamisho msimu huu huku timu kama Real Madrid, Inter Milan na Barcelona zikionyesha nia ya kutaka huduma zake.
Arshavin last week aliweka wazi kuwa anataka kubaki Emirates anasema kuwa ni vigumu kwa Fabregas kubaki Arsenal msimu ujao, "Fabregas mwishoni mwa msimu alitupa zawadi ambazo nilimuuliza ni kwa ajili ya kuagana lakini alishindwa ni kunijibu, na nafikiri kuna kitu nyuma ya ukimya ule".- Arshavin

Wakati taarifa kutoka Stamford Bridge zinasema kuwa mmiliki na tajiri wa Chelsea Roman Abromavich yupo tayari kulipa pesa ambayo Arsenal wanataka ili aweze kumleta Fabregas na kuwapiku Real Madrid, Barcelona na Inter ambao nao wanasaka saini wa kiungo huyo zao la academy ya Barca inayojulikana kama La Masia.

No comments:

Post a Comment