Search This Blog

Sunday, June 5, 2011

UTAPATA NAFASI YA KUCHEZA MAN U? - TONY MORLEY AMUULIZA YOUNG


Shujaa wa Aston Villa Tony Morley amezishangaa hekima za Ashley Young juu ya kutaka kwake kujiunga na Manchester United.

United ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumnyakua winga huyo mbele ya mahasimu wao Liverpool, lakini Morley ambaye aliwezesha Villa kunyakua kombe la European Cup mwaka 1982 ana wasiwasi kama Young atapata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha Fergie.

"Nafahamu anataka kucheza katika Champions League, lakini ndani ya kikosi cha United atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara? Naamini anataka kuwa moja ya wachezaji ndani ndani ya United lakini sidhani kama atatpata nafasi hiyo."

"Mfano mzuri ni James Milner si ameuona? ndio hali halisi atakayokutana nayo Young.Milner anaweza kusema ameshinda FA Cup lakini yeye alikuwa Benchi ndani ya kikosi cha Manchester City.Young ni mzuri sana lakini na uwezo mkubwa lakini hawezi kupata nafasi kubwa ya kucheza Old Trafford, atatakiwa kugombea nafsi dhidi ya Nani na Antonio Valencia hapo unaona ugumu wake". alisema Tony Morley


No comments:

Post a Comment