Search This Blog

Wednesday, May 11, 2011

TERRY-IT'S ALL OVER NOW


Baada ya jumapili kupokea kipigo kutoka kwa Man UTD, England and Chelsea captain John amesema ni vigumu kukubali ukweli lakini ubingwa wameshaukosa.

Chelsea ambayo jana ilienda Old Trafford ikijua ushindi pekee ndio ungeweka hai matumaini ya kuutetea ubingwa wao lakini magoli ya mapema kabisa ya Javier Hernandez "Chicharito" na Nemanja Vidic yalizima ndoto za watoto wa Abromavich.

Akiongea baada ya mechi John Terry alisema, "Sijui nini kilitokea, tulienda Old Trafford na matumaini na kuomba tuuanze mchezo vizuri lakini haikuwa hivyo.United walianza vizuri na kupata magoli ya mapema ambayo yaliwasaidia kujipanga vyema.Kipindi cha kwanza hatustahili chochote kwenye mchezo ule second half tulijitahidi tukacheza vizuri na kufanikiwa kupata goli moja lakini halikutosha kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa wetu."

1 comment:

  1. its all over, we brought our trophy back.
    Kilichobaki ni Sneidjer kutua OT na kuendelea kunenepesha akaunti ya makombe.

    ReplyDelete