Search This Blog

Wednesday, May 11, 2011

TEAM YA TAIFA YA AFRIKA KUSINI BAFANA BAFANA YATARAJIA KUSHUKA NCHINI.


Kikosi cha timu ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) kikiongozwa na kiungo wa Kaizer
Chiefs, Siphiwe Tshabalala kitawasili nchini Mei 12 mwaka huu saa 1.30 jioni kwa
ndege ya South African Airways kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars
itakayochezwa Mei 14 mwaka huu saa 12 kamili jioni Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.


Wachezaji wengine kwenye kikosi hicho kinachofundishwa na Pitso Mosimane ni
makipa: Itumeleng Khune na Wayne Sandilands. Mabeki ni Morgan Gould, Siyanda
Xulu, Eric Matoho, Mzivukile Tom, Prince Hlela, Siyabonga Sangweni, Tefu
Mashamaite na Siyanda Zwane.


Viungo ni Hlompho Kekana, Thanduyise Khuboni, Reneilwe Letsholonyane, Thandani
Ntshumayelo,Thabo Matlaba, Erwin Isaacs na Sifiso Myeni wakati washambuliaji ni
Bernard Parker, Vuyisile Wana, Lehlohonolo Majoro na Katlego Mphela.


WACHEZAJI WA STARS KUTOKA NJE
Klabu ya Vancouver Whitecaps imemnyima ruhusa Nizar Khalfan kwa vile Mei 15
mwaka huu itakuwa na mechi muhimu ya ligi. Ujio wa wachezaji Idrissa Rajab,
Henry Joseph, Abdi Kassim, Dan Mrwanda na Athuman Machupa bado tunafuatilia
majibu katika klabu zao.


Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zitaanza kuuzwa Alhamisi (Mei 12 mwaka huu)
katika vituo vya Premier Betting (Kariakoo- Mtaa wa Sukuma, Buguruni Sokoni,
Manzese Midizini, JM Mall na Tandale kwa Mtogole), Shule ya Sekondari Benjamin
Mkapa, Steers (Mtaa wa Ohio na Samora), Big Bon Msimbazi (Kariakoo) na Uwanja wa
Uhuru.

No comments:

Post a Comment