Search This Blog

Thursday, May 26, 2011

SIITEGEMEI KUITWA ENGLAND - MICHEAL OWEN


Michael Owen bado anaamini atapata mkataba mpya na Man United lakini ameshakata tamaa ya kuitwa na Fabio Capello in England squad.
Owen amepata medali yake ya kwanza ya EPL msimu huu, ingawa amekuwa akikalia benchi na inaaminika Ferguson atamwacha baada ya mkataba wake wa miaka kuisha lakini mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool, Newcastle na Real Madrid anasema bado anapenda kubaki Theatre Of Dreams.
The 31-year-old, ambaye alifunga bao lake la kwanza msimu kwenye ligi kuu dhidi ya Blackpool jumapili iliyopita alisema "Nataka kubaki Man United, ni klabu kubwa na nzuri, itabidi nifahamu ndani ya wiki mbili zijazo na nitaongea na Fergie."
"Kwa sasa nimeshakata tamaa ya kuchaguliwa kwenye timu ya taifa na Capello, sijaitwa kuichezea timu yangu tangu mechi ya kirafiki na Ufaransa miaka 3 iliyopita.Inaniuma kutoitumikia taifa langu lakini sina jinsi, mara nilipokoswa kuitwa nilisikita,mara pili pia, lakini baada ya mara 4 na zilizofuata sikuwahi kutegemea tena kuona jina langu on the board." alisema Micheal Owen.

No comments:

Post a Comment